WAZIRI BASHUNGWA: MAKANDARASI WABABAISHAJI KUCHUKULIWA HATUA. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, January 20, 2024

WAZIRI BASHUNGWA: MAKANDARASI WABABAISHAJI KUCHUKULIWA HATUA.

Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa, akisisitiza jambo kwa Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa, Sophia Kizigo (Wa Kwanza Kushoto), wakati Waziri huyo alipokagua ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami, kipande cha barabara ya Mbande- Kongwa Jct- Ng’ambi-Mpwapwa (Km 5) Tarehe 19 Januari, 2024 jijini Dodoma.
Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa, akizungumza na wananchi wa Mpwapwa Mjini mara baada ya kukagua ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami, kipande cha barabara ya Mbande- Kongwa Jct- Ng’ambi-Mpwapwa (Km 5) Tarehe 19 Januari, 2024 jijini Dodoma.
Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa, Sophia Kizigo, akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa, wakati Waziri huyo alipokagua ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami, kipande cha barabara ya Mbande- Kongwa Jct- Ng’ambi-Mpwapwa (Km 5) Tarehe 19 Januari, 2024 jijini Dodoma.

Baadhi ya wananchi wa Mpwapwa Mjini, jijini Dodoma, wakifurahi mara baada ya kuhakikishiwa na Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa, kuwa Ujenzi wa barabara ya Mbande – Kongwa Junction- Mpwapwa Sehemu ya Kongwa – Mpwapwa (Km 32) uko mbioni kuanza.
Mouonekano wa ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami, kipande cha barabara ya Mbande- Kongwa Jct- Ng’ambi-Mpwapwa (Km 5) jijini Dodoma, Tarehe 19 Januari, 2024.

Na Mwandishi Wetu, Mpwapwa 

Serikali imetoa onyo kali dhidi ya Makandarasi wababaishaji na kusisitiza hatua kali za kisheria kuchukuliwa kwa mkandarasi yeyote atakayekiuka miiko na maadili ya taaluma yake.

Onyo hilo limetolewa na Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa, wilayani Mpwapwa jijini Dodoma mara baada ya kukagua ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kipande cha Mbande - Kongwa Junction - Ng'ambi - Mpwapwa (km 5)

Aidha, Bashungwa amewaagiza Mameneja wa TANROADS katika mikoa yote nchini kuhakikisha kila mwezi wanaandaa orodha ya Makandarasi wababaishaji na kutuma Wizarani ili hatua stahiki dhidi yao kuchukuliwa mapema.

"Sitegemei kuona kuna Wakandarasi wababaishaji katika miradi ya TANROADS, ikibainika kuwepo kwa baadhi yao hakikisha Meneja unamchukulia hatua kali za kisheria kwa mujibu wa mkataba sitaki kuona hali ya Misenyi inajitokeza kwenye miradi ya TANROADS", amesema Bashungwa.

Amesisitiza kuzipima Bodi za Usajili wa wahandisi (ERB) na Bodi za Usajili wa Makandarsi (CRB) kwa kuhakikisha wanafuatilia miradi yote ambayo inasuasua na kuchukua hatua katika miradi hiyo.

Halikadhalika kuhusu ujenzi wa barabara ya Mbande - Kongwa -  Junction - Mpwapwa sehemu ya Kongwa Mpwapwa (Km 32) kwa kiwango cha lami, Waziri Bashungwa amesema kuwa Mkandarasi ameshapatikana na muda si mrefu serikali itasaini mkataba na ujenzi kuanza.

Kwa upande wake, Kaimu Meneja wa TANROADS mkoa wa Dodoma, Eng. Colman Gaston amesema kuwa ujenzi wa barabara sehemu ya Kongwa - Mpwapwa (km 32) inatarajiwa kujengwa na mkandarasi M/ S Estim Construction ambapo maandaliziya kutia saini mkataba wa ujenzi yanaendelea.

Naye, Mbunge wa Mpwapwa, Mhe. George Malima amesema kuwa imani ya wananchi wake ni kupata barabara ya lami na kusisitiza kuwa ni matarajio yake kuwa ahadi hiyo itatimia kwani imekuwa ni kilio cha muda mrefu kwa wilaya kongwe kama hiyo kukosa barabara ya lami.

"Wilaya hii ni kongwe ilianza tangu mwaka 1926 tunashangaa hadi leo haina barabara ya lami, tunaamini kuja kwako kutakuwa mkombozi katika wilaya hii", amesema Malima. 

No comments:

Post a Comment