Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Januari 19, 2024 ameshiriki ufunguzi wa mkutano wa 19 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa kundi la Umoja wa Nchi na Serikali 120 zenye Msimamo wa Sera ya Kutofungamana na Upande Wowote (NAM), Kampala nchini Uganda.
Waziri Mkuu amemuwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mkutano huo.
Katika mkutano huo Rais wa Jamhuri ya Cuba Miguel Mario Diaz-Canel Bermudez amemkabidhi rasmi Rais wa Uganda Yoweri Museveni uenyekiti wa kundi hilo.
No comments:
Post a Comment