KATIKA mwaka wa fedha 2023/24 Serikali imetenga kiasi cha Sh Milioni 100 kwa ajili ya ukamilishaji wa jengo la wazazi na upasuaji, ujenzi wa vyoo pamoja na ujenzi wa kichomea taka katika Kituo cha Afya Migoli kilichopo wilayani Iringa.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI anayeshughulikia afya, Mhe Dkt Festo Dugange wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Mhe Grace Tendega aliyehoji ni lini serikali itamalizia ujenzi wa kituo hicho.
“ Katika mwaka wa fedha 2021/22, Serikali ilipeleka Sh Milioni 400 katika Halmashauri ya Iringa kwa ajili ya ujenzi wa majengo matatu ya Kituo cha Afya Migoli. Ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje (OPD) umekamilika na linatoa huduma. Jengo la wazazi na upasuaji yako asilimia 90 ya ukamilishaji,” Amesema Mhe Dkt Dugange.
No comments:
Post a Comment