NAHODHA WA NIGERIA NJE MSIMU MZIMA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, February 28, 2024

NAHODHA WA NIGERIA NJE MSIMU MZIMA




Mchezaji wa Nigeria William Troost-Ekong anatazamiwa kufanyiwa upasuaji na atakosa msimu uliosalia baada ya kupata jeraha kwenye AFCON 2023.

 

Nahodha huyo wa timu ya taifa ya Nigeria aliwasili Finland kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji mdogo wa kutibu misuli ya paja la kulia.

 


Mwandishi wa habari wa Nigeria Oluwashina Okeleji alifichua kwa BBC kwamba mchezaji huyo anaugua maumivu ya misuli ya paja aliyopata wakati wa Kombe la Mataifa ya Afrika.




 Troost-Ekong alipata jeraha hili katika raundi ya pili ya hatua ya makundi ya AFCON 2023, katika mchezo kati ya Nigeria na Ivory Coast. Licha ya kushindwa, William alishinda tuzo ya MVP wa mashindano hayo.

 

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 alifanikiwa kufunga mara tatu wakati wa michuano hiyo, likiwemo bao katika fainali, kabla ya Nigeria kushindwa na Ivory Coast na The Eagles kupata medali ya fedha.


Nahodha huyo wa Nigeria anatarajiwa kufanyiwa upasuaji nchini Finland siku ya Jumanne kukarabati biceps femoris iliyopasuka ndani mguu wake wa kulia.






No comments:

Post a Comment