"PANDENI MITI KATIKA MAENEO MLIYOPO" - ACP OTIENO - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, February 8, 2024

"PANDENI MITI KATIKA MAENEO MLIYOPO" - ACP OTIENO


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Martine Otieno ameongoza Maofisa Wakaguzi na Askari wa vyeo mbalimbali katika zoezi la upandaji wa Miti zaidi ya miambili katika eneo la kambi ya Polisi Nzuguni Jijini Dodoma February 07, 2024.

Kamanda Otieno amewataka Askari kuwa na utamaduni wa kutunza mazingira, kuzingatia usafi ili kuepukana na magonjwa ya milipuko ikiwemo kipindupindu pamoja na kupanda miti katika maeneo wanayoishi ili kunufaika nayo.


Katika hatua nyingine Mkuu Wa Polisi Jamii Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Wa Polisi (ACP) Eva Stesheni amesema zoezi la upandaji wa miti ni moja ya miradi ya Polisi hivyo kila Askari anapaswa kushiriki katika zoezi hilo pamoja na kuunga mkono juhudi za serikali katika ajenda ya kuikijanisha Dodoma.

Toka: Dawati la habari Dodoma.


No comments:

Post a Comment