![]() |
| Ujumbe wa Tanzania ukifuatilia mijadala katika kikao cha mwisho cha mijadala cha Mawaziri wa Fedha na Afya wa SADC uliofanyika Harare, Zimbabwe. |
![]() |
| Picha ya pamoja ya ujumbe wa Tanzania mara baada ya kumalizika kwa mijadala ya Mawaziri wa Fedha na Afya wa SADC uliofanyika Harare, Zimbabwe. |
Leo Julai 3, 2026, ilikuwa siku ya mwisho ya Mkutano wa Kamati ya Mawaziri wa Fedha na Uwekezaji wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), ambapo nchi wanachama zilihitimisha majadiliano kwa kuwasilisha hoja, mapendekezo na maazimio yaliyolenga kuimarisha ushirikiano wa kikanda katika sekta za fedha, uwekezaji, afya, maendeleo ya masoko ya mitaji na uthabiti wa uchumi wa Kanda. Maamuzi ya mkutano huo yanatarajiwa kuwasilishwa kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC unaotarajiwa kufanyika mwezi Agosti, 2026 Durban, Afrika Kusini kwa ajili ya kuridhiwa ili maamuzi hayo yaanze kutekelezwa.
Katika mjadala wa mwisho, wajumbe walisisitiza umuhimu wa kuendelea kuoanisha sera za fedha na uwekezaji, kuimarisha mifumo ya ukusanyaji wa rasilimali fedha na maendeleo, pamoja na kuongeza ushirikiano katika kukabiliana na changamoto zinazoikabili kanda ili kufanikisha malengo ya Dira ya SADC 2050 na Mpango wa Kimkakati wa Maendeleo wa Kanda –(Reginal Indicative Strategic Development Plan -RISDP 2020–2030).
Mkutano huo ulihudhuriwa na wajumbe kutoka nchi zote 16 wanachama wa SADC ambazo ni Angola, Botswana, Comoro, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Eswatini, Lesotho, Madagascar, Malawi, Mauritius, Msumbiji, Namibia, Shelisheli, Afrika Kusini, Tanzania, Zambia na Zimbabwe.






No comments:
Post a Comment