Na Okuly Julius-Dodoma
Mafundi Rangi na Ujenzi takribani 1000 Jijini Dodoma wamepatiwa Mafunzo yenye lengo la kuwapa mbinu za kisasa za ujenzi na matumizi ya vifaa mbalimbali vinavyostahili katika kukamilisha shughuli zao.
Akizungumza kwenye semina hiyo Mkurugenzi wa RockMax international Limited Hamoud Abdallah amesema kuwa semina hii ya mafundi kwa Mkoa wa Dodoma ni kwa rika zote walioajiriwa na waliojiajiri ikiwemo mafundi wa Serikali na kutoka sekta mbalimbali.
"Mafundi waliohudhuria hapa ni takribani mafundi 1000 na hii ni matumaini ya kwamba wataenda kuwa mabalozi wazuri na kufundisha wengine huko katika maeneo yao ya Kazi"amesema
Ameongeza kuwa yote haya ni kuhakikisha tunaongeza uwezo kwa vijana na rika mbalimbali katika kujiajiri,na maarifa haya yametolewa kwa wote ikizingatia jinsia zote bila upendeleo.
Aidha amesema kuwa wao RockMax international Limited wazalishaji wa Extra power skimming putty wamejitoa na kuwa karibu na Chama cha Mafundi cha Tanzania (CHAMARAUTA) katika kuhakikisha thamani na umuhimu wao na maendeleo yao kwa pamoja ni kipaumbele chetu.
"Tuko nao pamoja katika kudhamini harakati zao mbalimbali ili kuhakikisha mafundi wanafikia malengo yao"Amesema
Katika hatua nyingine Mkurugenzi huyo wa RockMax international Limited amemwomba Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kuhakikisha anawapigia Debe Chama Cha mafundi ili waweze kukumbukwa na kupatiwa fursa zaidi katika Kazi na miradi mbalimbali ya serikali na miradi ambayo serikali imeingia ubia kwa Mashirika binafsi.
Naye Mkurugenzi wa DUDA Development Foundation Peter Dafi kwa upande wake amesema kwenye semina ya Leo wamewafundisha Mafundi kuhakikisha wanakuwa na ufundi bora wa majengo yetu tunayoishi
"Ili jengo liwe bora fundi anapaswa azingatie mambo mbalimbali ya msingi"Amesema
Aidha amewasisitiza mafundi hao kuwa na nidhamu kwa kila jambo wanalolitenda,ili kuweza kuzifanya kazi zao kwa ufasahaa.
Akizungumza kwenye semina hiyo Mgeni rasmi ambae ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule ametoa wito kwa mafundi hao kuhakikisha wanafanya Kazi kwa ubora
"Majengo yanayojengwa Dodoma,Dodoma ni Makao Makuu ya nchi liwe Jengo la mtu binafsi liwe Jengo la Serikali yawe majengo ambayo yana viwango,kwa hiyo nyie ndo mnaotuwekea vile viwango"Amesema
Ameongeza kuwa tusaidieni kufanya kazi kwa ubora unaotakiwa zile rangi zinazowekwa baadae zinaanza kubanduka hatutegemei kutoka kwa mafundi Wazuri kama ninyi.
Aidha ametoa wito kwa mafundi ambao hawajajiunga na Chama Cha mafundi rangi na Ujenzi (CHAMARAUTA)kuweze kujiunga na Chama hicho ili waweze kupata nguvu ya kujitetea
Pia Senyamule ametoa wito kwa kampuni nyingine ziweze kuiga mfano wa RockMax international kwa kurudisha fadhila kwa wale wanaowahudumia au wanaofanya nao biashara kwa sababu ni mfano mzuri.
No comments:
Post a Comment