Na Okuly Julius , Dodoma
MAMLAKA ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) ,inaendelea na jitihada za kuhakikisha wanatekeleza mradi wa Majisafi na Majitaka katika Mji wa Serikali Mtumba (MAGUFULI CITY).
Ili kuhakikisha mradi huo unakamilika , leo Machi 22,2024 wakati wa kilele cha wiki ya maji kitaifa na siku ya maji duniani , DUWASA imesaini mikataba mitatu tofauti yenye wakandarasi watatu ikiwa na thamani ya Zaidi ya Bilioni 87.6 (Bila VAT) huku Mhandisi mshauri aliyesanifu mradi huo ambaye pia atakuwa msimamia wa ujenzi wa mradi huo atagharimu Zaidi ya Tsh bilioni 1.28 (Ikiwa na VAT) na muda wa mradi huo ni mwaka mmoja baada ya malipo ya awali kukamilika.
Ambapo Mkataba wa Kwanza utahusisha Utafiti wa maji ardhini kupata vituo 8 vyenye uwezekano wa kupatikana maji ,uchimbaji wa wa visima walau vinne vya kuzalisha maji vyenya kina cha 150m kila kisima,ujenzi wa tanki la kuhifadhi maji kwa muda (water sump) lenye ujazo wa mililita 1000 na tank la kuhifadhi maji (storage tank) yenye ujazo wa mililita 5000 na ujenzi wa mfumo wa majisafi yenye jumla ya umbali wa Kilometa 12.3 na utatekelezwa na Kampuni ya China Railways Seventh Group Ltd kwa gharama Zaidi ya Bilioni 35.63 za Kitanzania (Bila VAT)
Mkataba wa Pili ni Ujenzi wa mtandao wa kusafirisha Majitaka toka kwenye majengo kuelekea kwenye bomba kubwa (trunk main) kwa Km 39.3 (DN 225 – 250mm) mradi huu utatekelezwa na Kampuni ya China Harbour Engineering Ltd kwa zaidi ya gharama ya Tsh Bilioni 20.02 (Bila VAT)
Mkataba wa Tatu ni Ujenzi wa Mabwawa 10 ya kutibu Majitaka na ujenzi wa bomba kubwa la majitaka lenye ukubwa wa (250 - 560mm) na umbali wa km 15.1 na utatekelezwa na Kampuni ya Beijing Construction Engineering Ltd , kwa zaidi ya Bilioni 31.94 za kitanzania (Bila VAT)
Mikataba hiyo Mitatu imesainiwa mbele ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko na Waziri wa Maji Jumaa Aweso katika maadhimisho ya kilele cha wiki ya maji Kitaifa na Siku ya Maji Duniani.
No comments:
Post a Comment