Msako mkali unaendelea kumtafuta mtoto wa miaka sita Joslin Smith, aliyetoweka tarehe 19 Februari. |
Joslin Smith alitoweka kutoka nje ya nyumba yao huko Saldanha Bay, karibu na Cape Town, wiki mbili zilizopita.
Maafisa hao 300 wa wanamaji wanaungana na waokoaji kutoka Jiji la Cape Town, kitengo cha mbwa na ndege zisizo na rubani katika msako huo bila kukata tamaa.
Wengi wanauliza kwa nini bado hajapatikana? Kwani watoto hupotea kila baada ya saa tano nchini Afrika Kusini, lakini wengi hupatikana.
Wachunguzi wana uhakika wa mafanikio baada ya nguo zilizokuwa na damu kupatikana katika uwanja wa wazi uliopo karibu.
Vitu hivyo vilivyogunduliwa siku ya Jumamosi, vimepelekwa kwenye maabara ya uchunguzi zaidi.
Msemaji wa polisi Brigedia Novela Potelwa aliambia BBC kuwa maafisa wa wanamaji walitumwa siku ya Jumatatu kusaidia kufuata mkondo wowote.
Sio kawaida kwa jeshi la wanamaji kusaidia katika upekuzi wa raia lakini wanaweza kufanya hivyo wakiulizwa na polisi.
Meya wa Saldanha Bay André Truter alitabiri kuwa itakuwa "siku kuu" kwa shughuli za utafutaji.
"Nilisimama kwa mshangao nilipoona jinsi watu wengi kutoka mashirika mengi tofauti, wakiongozwa na SAPS [Huduma ya Polisi ya Afrika Kusini], wakilenga katika kufanikisha kazi hiyo! Ilinipa matumaini mapya ya kumpata mtoto Joslin," Bw Truter alisema.
Wanajamii waliochanganyikiwa walipekua mabomba ya maji taka na mashimo katika eneo lote siku chache baada ya kutoweka kwa msichana huyo, huku umati wa watu wenye hasira pia wakienda kwenye nyumba za upekuzi na kuwaandama majirani, alisema Bw Truter.
Zawadi ya randi 100,000 (13,260,637.84TZS) imetolewa kwa yeyote aliye na taarifa kuhusu mahali alipo, huku mitandao ya kijamii ikijaa matumaini na maombi kwamba Joslin atapatikana akiwa hai.
Aliachwa chini ya uangalizi wa mpenzi wa mam yake, Jacquin Appollis, katika makazi yasiyo rasmi, alipotoweka.
Hakuweza kueleza aliko, polisi walisema.
Hata hivyo, amekana kuhusika katika kutoweka kwake.
Mama yake Joslin aliambia jarida la ndani la The Daily Voice kwamba kamwe hakati tamaa.
"Mimi silika yangu ya kimama inaniambia binti yangu bado yuko hai na eneo hili tutampata, nitatembea kwa miguu kumtafuta. Nitaangalia kwenye kila kibanda, nitafanya peke yangu ikiwa lazima iwe."
Wanandoa hao wameshutumiwa na baadhi ya wanajamii kwa kuhusika na kutoweka kwa binti yao, shtaka ambalo wote wawili wamelikanusha.
Tangu wakati huo wamehamishwa hadi kwenye hifadhi kwa usalama wao wenyewe.
Brig Potelwa alisema umma haupaswi kueneza habari za uwongo kuhusu kutoweka kwa Joslin au kushiriki rekodi kutoka kwa shughuli za upekuzi.
"Hii inaweza kuathiri vibaya uchunguzi. Lengo kuu la juhudi zilizoratibiwa linapaswa kuwa kumtafuta Joslin au kile kilichomtokea."
No comments:
Post a Comment