LISHE BORA MSINGI MUHIMU KWA MAENDELEO YA WANAFUNZI – DKT. RWEZIMULA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, March 1, 2024

LISHE BORA MSINGI MUHIMU KWA MAENDELEO YA WANAFUNZI – DKT. RWEZIMULA

NAIBU Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt.Franklin Rwezimula,akizungumza wakati wa Maadhimisho ya siku ya Afrika ya chakula shuleni yaliyoandaliwa na Wizara hiyo kwa kushirikiana na wadau kutoka Shirika la Global Communities kupitia mradi wa Pamoja Tuwalishe na Shirika la Sanku yaliyofanyika leo Machi 1,2024 jijini Dodoma.
MKURUGENZI Msaidizi Uendelezaji Sera Elimu Msingi Bw.Victor George,akizungumza wakati wa Maadhimisho ya siku ya Afrika ya chakula shuleni yaliyoandaliwa na Wizara hiyo kwa kushirikiana na wadau kutoka Shirika la Global Communities kupitia mradi wa Pamoja Tuwalishe na Shirika la Sanku yaliyofanyika leo Machi 1,2024 jijini Dodoma.
MTHIBITI Ubora wa Shule Kanda ya Kati Bi.Nanzia Abdu Mahuna,akizungumza wakati wa Maadhimisho ya siku ya Afrika ya chakula shuleni yaliyoandaliwa na Wizara hiyo kwa kushirikiana na wadau kutoka Shirika la Global Communities kupitia mradi wa Pamoja Tuwalishe na Shirika la Sanku yaliyofanyika leo Machi 1,2024 jijini Dodoma.
MKURUGENZI wa Elimu TAMISEMI Dkt.Emmanuel Shindika,akizungumza wakati wa Maadhimisho ya siku ya Afrika ya chakula shuleni yaliyoandaliwa na Wizara hiyo kwa kushirikiana na wadau kutoka Shirika la Global Communities kupitia mradi wa Pamoja Tuwalishe na Shirika la Sanku yaliyofanyika leo Machi 1,2024 jijini Dodoma.
BAADHI ya Wadau wa Elimu wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt.Franklin Rwezimula (hayupo pichani),akizungumza wakati wa Maadhimisho ya siku ya Afrika ya chakula shuleni yaliyoandaliwa na Wizara hiyo kwa kushirikiana na wadau kutoka Shirika la Global Communities kupitia mradi wa Pamoja Tuwalishe na Shirika la Sanku yaliyofanyika leo Machi 1,2024 jijini Dodoma.
BAADHI ya Wanafunzi wakisikiliza hotuba ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt.Franklin Rwezimula (hayupo pichani),akizungumza wakati wa Maadhimisho ya siku ya Afrika ya chakula shuleni yaliyoandaliwa na Wizara hiyo kwa kushirikiana na wadau kutoka Shirika la Global Communities kupitia mradi wa Pamoja Tuwalishe na Shirika la Sanku yaliyofanyika leo Machi 1,2024 jijini Dodoma.
BAADHI ya Wanafunzi wakisikiliza hotuba ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt.Franklin Rwezimula (hayupo pichani),akizungumza wakati wa Maadhimisho ya siku ya Afrika ya chakula shuleni yaliyoandaliwa na Wizara hiyo kwa kushirikiana na wadau kutoka Shirika la Global Communities kupitia mradi wa Pamoja Tuwalishe na Shirika la Sanku yaliyofanyika leo Machi 1,2024 jijini Dodoma.

               MRATIBU wa Lishe kutoka Wizara ya Elimu ,Sayansi na Teknolojia Bi.Grace Shileringo,akizungumza na waandishi wa habari wakati wa Maadhimisho ya siku ya Afrika ya chakula shuleni yaliyoandaliwa na Wizara hiyo kwa kushirikiana na wadau kutoka Shirika la Global Communities kupitia mradi wa Pamoja Tuwalishe na Shirika la Sanku yaliyofanyika leo Machi 1,2024 jijini Dodoma. NAIBU Mkurugenzi wa Shirika la Global Communities wanaotekeleza mradi wa Pamoja Tuwasilishe, Vick Macha,akizungumza na waandishi wa habari wakati wa Maadhimisho ya siku ya Afrika ya chakula shuleni yaliyoandaliwa na Wizara hiyo kwa kushirikiana na wadau kutoka Shirika la Global Communities kupitia mradi wa Pamoja Tuwalishe na Shirika la Sanku yaliyofanyika leo Machi 1,2024 jijini Dodoma. NAIBU Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt.Franklin Rwezimula,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuzungumza wakati wa Maadhimisho ya siku ya Afrika ya chakula shuleni yaliyoandaliwa na Wizara hiyo kwa kushirikiana na wadau kutoka Shirika la Global Communities kupitia mradi wa Pamoja Tuwalishe na Shirika la Sanku yaliyofanyika leo Machi 1,2024 jijini Dodoma.


 Na Okuly Julius, Dodoma


Imeelezwa Lishe Bora Shuleni imekuwa msingi muhimu katika maendeleo ya wanafunzi , huku ikichangia kupata uwezo mzuri katika ufundishaji na ujifunzaji.


Akizungumza katika Maadhimisho ya Siku ya Afrika ya Chakula Shuleni leo Machi 1,2024 jijini Dodoma Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Dkt. Franklin Rwezimula amesema Waraka wa Elimu namba 3 wa Mwaka 2016 unaohusu utekelezaji wa elimu bila ada umeainisha majukumu ya kila mdau wakiwemo waziza.


 Dkt. Rwezimula amesema pamoja na umuhimu wa wananfunzi kupata chakula shuleni , yapo madhara yanayotokea kwa wanafunzi wanapokosa chakula shuleni ikiwemo kukabiliana na njaa,kukosekana kwa usikivu wakatai wa ujifunzaji ,utoro wa rejereja na hata kukatisha masomo kwa baadhi ya wanafunzi.


Pamoja na majukumu mengine jukumu mojawapa la mzazi katika waraka huo ni kushirikiana na shule kwa kuchangia upatikanaji wa huduma ya chakula kwa wanafunzi na serikali kuendelea kutekeleza majukumu yake kama ilivyoainishwa katika waraka huo.


“Kwa mara ya kwanza nchi yetu imeungana na mataifa mengine Afrika kuadhimisha siku hii muhimu ya chakula na lishe kwa wanafunzi ,napenda kupongeza juhudi za serikali yetu chini ya Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji mkubwa unaofanyika katika sekta ya elimu ili kuhakikisha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji yanavutia na maono haya yanatupa chachu na nguvu ya kufanya kazi kwa bidii ili kuhakikisha watoto wa Kitanzania wanapata elimu bora na jumuisha kwa wote,” amesema Dkt. Rwezimula


Kwa upande wake Mratibu wa Lishe kutoka Wizara ya Elimu ,Sayansi na Teknolojia, Bi. Grace Shileringo, ameipongeza serikali kwa kuendelea kuchagiza masuala ya Lishe na kuweka mikakati mbalimbali ya kuhakikisha jamii nzima inashirika katika kuchangia chakula ili watoto wapate lishe bora shuleni ikiwa ni pamoja na kuwaelimisha wazazi juu ya umuhimu wa wanafunzi kupata chakula.


“kwa sasa wazazi wengi wamehamasika kuchangia na kushirikiana na shule kuhakikisha watoto wanapata chakula shuleni wakiamini kuwa kufanya hivyo itawasaidia wanafunzi kuwa na utulivu wakati wakiwa Darasani," amesema Shileringo 


Ameongeza kuwa Wanachofanya wazazi na wadau mbalimbali ni kuhamisha tu ule mlo wa mchana kwa motto badala ya kula nyumbani basi apate chakula cha mchana shuleni ili aweze kuhudhuria masomo yake vizuri.


Naye Naibu Mkurugenzi wa Mradi wa PAMOJA TUWALISHE Bi. Vick Macha kutoka Shirika la Global Communities amesema wamekuwa wakitekeleza utoaji wa chakula Mashuleni kwa takribani miaka 10 wakihudumia katika mikoa ya Dodoma na Mara.


“Tumekuwa wadau wa muhimu sana katika eneo hili la lishe mashuleni na tunaishukuru Serikali kupitia Wizara ya elimu,sayansi na Teknoliojia na OR-TAMISEMI kwa kuendelea kushirikiana nasi katika eneo hili muhimu la Lishe mashuleni ili kuendelea kuwasaidia wanafunzi wetu wawapo shuleni,”


Maadhimisho ya Siku ya Afrika ya Chakula Shuleni (Africa Day of School Feeding) yamekuwa yakiadhimishwa kila mwaka barani Afrika ambapo mwaka huu kikanda yanaadhimishwa nchini Burundi ikibebwa na Kaulimbiu isemayo “Uwekezaji katika huduma ya chakula na lishe shuleni huchangia matokeo bora ya kielimu”



 

No comments:

Post a Comment