Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Mwajuma Waziri mapema leo amekabidhiwa majukumu ya ofisi yake na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Prof. Jamal Katundu
Katika hafla hiyo Prof. Katundu amemshukuru Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kumuamini kwa muda wote aliofanya kazi Wizara ya Maji.
Prof. Katundu amewataka watumishi wote wa Wizara ya maji kumpa ushirikiano wa kutosha Mhandisi Mwajuma pia kuishi kwa kufuata maadili katika utumishi wa umma ilikuweza kutimiza lengo la" kumtua mama ndoo ya maji kichwani"
No comments:
Post a Comment