PROF. MKUMBO AZITAKA MAMLAKA ZA MAJI KUPAMBANA NA UPOTEVU WA MAJI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, March 20, 2024

PROF. MKUMBO AZITAKA MAMLAKA ZA MAJI KUPAMBANA NA UPOTEVU WA MAJI


Na Okuly Julius , Dodoma

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji,Prof. Kitila Mkumbo, amezitaka Mamlaka za Maji nchini kwa kushirikiana na wataalam katika sekta ya maji,kuhakikisha wanazuia tatizo la upotevu wa Maji ili kuiondolea hasara Serikali inayotokana na upotevu huo.

Prof. Mkumbo,ametoa maagizo hayo Leo Machi 20 Jijini Dodoma wakati akizungumza na watendaji mbalimbali wa Sekta ya Maji wakiwemo Wadau wa Maji ,katika Kikao kazi kuhusu mapitio ya Sekta ya Maji yenye lengo la kujipima maendeleo kwa kazi wanazofanya.

Sanjari na hilo,Waziri Mkumbo,amesema lengo la Dira ya maendeleoya Tifa ni kukuza uchumi ivyo kipaumbel cha Rais ni ajenda ya Maji ni kuhakikisha watu wote wanapata Maji huku akiwataka watumishi wa Wizara ya Maji katika Taarifa zao za Mwaka wazingatie suala la kuwekeza kwenye miundombinu ya Maji.


Pia amezungumzia hali ya upatikanaji wa maji kuwa  imezidi kuongezeka mjini na vijijini na kwa kasi ilivyo, malengo yaliyowekwa na serikali yatafikiwa asilimia 85 vijijini na 95 mijini.

"Takwimu za hali ya upatikanaji wa maji inatokana na uwekezaji unaofanywa na serikali katika kufikisha huduma ya maji kwa wananchi" alisema.

Amesema lengo kubwa la Serikali ni kukuza uchumi shindani na kuleta maendeleo ya watu na huduma ya maji ni moja ya jambo muhimu katika kufanikisha hatua hiyo hapa nchini.

“Watendaji wa Sekta ya Maji wanafanya kazi kubwa na nzuri, tena usiku na mchana kwa ajili ya wananchi” alisema Prof.Kitila.

Waziri Kitila amesema kuwa Waziri wa Maji halali akipambania masuala ya maji kufika katika makazi ya wananchi.

Mhe.Prof.Kitila amesisitiza suala la upotevu wa maji (NRW) lifanyiwe kazi zaidi kwa sababu linaongeza gharama za uendeshaji na Wakurugenzi wa Mamlaka za Maji wapimwe katika hatua wanazochukua kuzuia upotevu wa maji.

Aidha,Prof.Kitila ameipongeza kazi ya utunzaji na uendelezaji wa vyanzo vya maji hapa nchini hatua ambayo moja ya matunda yake ni kujaa mapema kwa maji katika bwawa la kufua nishati ya umeme la Nyerere, kabla ya muda uliokisiwa ambapo kazi kubwa iliyofanywa na wataalamu wa Sekta ya Maji ni moja ya hatua zilizoitoa Tanzania kimasomaso katika mradi huo mkubwa.


Naye Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Maji (NWF) Haji Nandule amekabidhi hundi ya shilingi milioni 800 kwa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Bunda baada ya kuwa mamlaka ya kwanza kukidhi vigezo vya mkopo nafuu unaotolewa kwa ushirikiano na Benki ya Uwekezaji (TIB).

NWF inatoa fedha za utekelezaji wa miradi ya maji hapa nchini na imefungua dirisha la mikopo ya masharti nafuu kwa kushirikiana na Benki ya TIB.


Kwa upande wake,Mratibu Mkuu wa Wizara ya Maji,Remigius Mazigwa ameeleza program mbalimbali walizozifanya huku akitoa takwimu kuwa zaidi ya watu wanaugua magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindupindu kutokana na kukosa maji safi.

No comments:

Post a Comment