RAIS MUSEVENI AMTEUA MTOTO WAKE KUWA KAMANDA MKUU WA JESHI. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, March 22, 2024

RAIS MUSEVENI AMTEUA MTOTO WAKE KUWA KAMANDA MKUU WA JESHI.


Rais Yoweri Museveni wa Uganda ambaye pia ni amiri jeshi mkuu amefanya mabadiliko katika jeshi la Uganda (UPDF)na kumrejesha mwanae Lt.Jenerali Muhoozi Kainerugaba kuwa mkuu wa kikosi cha ulinzi wa rais yaani Special Force Command(SFC) Mabadiliko hayo yamefanyika wakati wanasisa wa upinzani wakilaumu jeshi la polisi kwa kuwasumbua katika kampeni zao za uchaguzi zinazoendelea nchini.


Aliyekuwa naibu wa mkuu wa jeshi la polisi IGP Meja Jenerali Sabiiti Muzeyi na nafasi hiyo imechukuliwa na Gen Paul Lokech aliyekuwa katika uangalizi maalum wa masuala ya Sudani kusini, ikiwa Sabiiti Muzeyi amerudishwa makao makuu ya jeshi kusubiri kupewa nafasi nyingine.

Muhoozi Kainerugaba anachukua nafasi ya Jenerali Wilson Mbasu Mbandi ambaye ameteuliwa kuwa waziri wa biashara katika mabadiliko mapya ya baraza la mawaziri yaliyotangazwa jana jioni.

Jenerali Mhoozi amerudishwa kwenye cheo ambacho aliwahi kukitumikia kabla ya kubadilishwa kuwa mshauri wa rais Museveni katika masuala ya ulinzi.Na kitengo hicho ndicho kina husika na kumulinda rais wa Uganda.


Mabadiliko haya yamefanyika wakati zikiendelea kampeni za uchaguzi mkuu wa rais ambapo wanasiasa wa upinzani wamekuwa wakituhumu jeshi la polisi kuwatatiza kwenye kampeni zao,lakini Msemaji wa jeshi amesema ni mabadiliko ya kawaida tu.


Katika uteuzi huo rais Museveni amemubakiza mkuu wa jeshi la polisi IGP Okoth Ochola kuhifadhi wadhifa wake.


Muhoozi aliwahi kuwa kwenye nafasi ya Ukamanda wa Jeshi la Ardhini la Uganda kabla ya kuondolewa kwenye nafasi hiyo mnamo Oktoba 04, 2022 huku nafasi yake ikichukuliwa na Meja Jenerali Kayanja Muhanga ambaye alikuwa Kamanda wa Operesheni Shujaa inayoendeshwa Nchini DRC.


Muhoozi Kainerugaba (katikati) akivalishwa cheo kipya cha Luteni Jenerali katika makao makuu ya Jeshi la Ulinzi la Uganda (UPDF) mjini Mbuya, kusini mashariki mwa Kampala.


No comments:

Post a Comment