BASHUNGWA AWASILI WILAYANI MAFIA KWA ZIARA YA KIKAZI. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, March 22, 2024

BASHUNGWA AWASILI WILAYANI MAFIA KWA ZIARA YA KIKAZI.


Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa (Mb) amewasili wilayani Mafia mkoani Pwani kufanya ziara ya kikazi ambapo amepokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Mafia, Aziza Mangosongo, leo tarehe 22 Machi 2024.

Bashungwa amepokelewa pia na Mbunge wa Mafia ambaye pia ni Naibu Waziri wa Elimu, Omary Kipanga pamoja na viongozi wa Serikali na Chama Cha Mapinduzi.

Katika ziara hiyo, Waziri Bashungwa atakagua miundombinu ya barabara ikiwa ni pamoja na Barabara ya Kilindoni - Kigamboni, barabara ya Kilindoni - Utende, Kivuko cha Kilindoni pamoja na kufanya mkutano wa hadhara Kirongwe.

No comments:

Post a Comment