Uzinduzi wa jengo la Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa Kikombo umefanyika leo Februari 24, 2026, ambapo Mgeni Rasmi alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Jiwe la msingi la ujenzi huo liliwekwa na Rais wa Awamu ya Tano, Hayati Dkt. John Pombe Magufuli, mnamo Novemba 25, 2019, huku ujenzi rasmi ukianza Machi 10, 2020.
Jengo hilo la kisasa linajumuisha ofisi zote za Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), likiwa na miundombinu muhimu na ya kisasa inayokidhi mahitaji ya kiutendaji kwa viwango vya juu.
Hadi kukamilika kwa awamu ya kwanza, mradi huo umegharimu zaidi ya Shilingi bilioni 121 za Kitanzania. Inatarajiwa kuwa kukamilika kwa awamu zote za ujenzi kutagharimu zaidi ya Shilingi bilioni 318.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na JKT, Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe, wazo la ujenzi wa jengo hilo lilianza tangu mwaka 1964 na kuingizwa rasmi katika mpango wa ujenzi mwaka 1974.






No comments:
Post a Comment