Ashrack Miraji Same Kilimanjaro
Kuelekea Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Mkoani Kilimanajaro Aprili 02,2024 Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Nurdin Babu amewataka viongozi na madereva wa bajaji na Bodaboda kutoa ushirikiano katika huduma ya usafiri iliyobora kwa wageni wanaotarajiwa kufika Mkoani hapo.
Amesema hayo Machi 19,2024 wakati wa kubandika vipeperushi (stiker) zenye ujumbe wa Uzinduzi wa Mbio za Mwenge kwenye bajaji katika kituo cha KCMC na kukabidhi viongozi wa Bajaji vipeperushi kwa ajili ya kusambaza kwenye bajaji zote.
Aidha, Katibu Tawala Mkoa wa Kilimanjaro Bw. Tixon Nzunda amesema Mkoa huo umepewa heshima ya kuzindua Mwenge wa Uhuru mwaka huu hii ni kutokana na Mwenge wa Uhuru kutimiza miaka 60 tangu kupandishwa kilele cha Mlima Kilimanjaro na kuanza rasmi kwa mbio,vile vile Taifa kutimiza miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar pamoja na miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar na miaka 25 ya kumbukizi ya Muasisi wa Taifa Baba wa Taifa Mwl. Julias Kambarage Nyerere tangu atutoke.
No comments:
Post a Comment