Wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya kimataifa, Simba na Yanga wamepewa waamuzi wa bahati kwa mwenyeji kwenye michezo yao ya robo fainali ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambayo watacheza wikiendi ijayo.
Shirikisho la soka Afrika (CAF), limewatangaza Abongile Tom, raia wa Afrika Kusini, kuwa ndiye atakayechezesha mchezo kati ya Simba na AI Ahly, Ijumaa ya Machi 29 huku Amin Omar wa Misri akichezesha mechi ambayo itachezwa Jumamosi ya Machi 30 kati ya Yanga na Mamelodi Sundowns.
Waamuzi hao wanaonekana kuwa na bahati kwa wenyeji wa michezo ambayo wamekuwa wakichezesha hivyo huenda Simba na Yanga zikabebwa na hillo.
Katika michezo 10 iliyopita ambayo Abongile amechezesha, wenyeji wameshinda mara saba, ushindi huo ni kwa asilimia 70 huku wakipoteza mara tatu sawa na asilimia 30, mwamuzi huyo ndani ya mechi hizo, amechezesha michuano mitatu tofauti ambayo ni Ligi ya Mabingwa, Kombe la Shirikisho na African Football League.
Aidha, hii itakuwa mara ya tatu kwa mchezo wa Simba kuchezeshwa na mwamuzi huyo, mara ya kwanza ilikuwa Desemba 2023 Mnyama akiwa ugenini (Morocco) alipoteza kwa bao 1-0 dhidi ya Wydad Casablanca.
Mechi nyingine ilikuwa Oktoba 16, 2022 lakini safari hiyo, Simba iliibuka na ushindi wa bao 1-0 kwenye uwanja wa Benjamini Mkapa, Abongile aliwahi
kuchezesha mechi ya Yanga ambayo Wananchi wallibuka na ushindi wa mabao 2-0 wakiwa ugenini dhidi ya Rivers United ya Nigeria kwenye Kombe la Shirikisho.
No comments:
Post a Comment