THABITI ALLY 'REAL JIMMY' AFUNGUKA JUU YA KIFO CHA MZEE WA MJEGEJE. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, March 20, 2024

THABITI ALLY 'REAL JIMMY' AFUNGUKA JUU YA KIFO CHA MZEE WA MJEGEJE.


Thabiti Ally Kipwasa 'Real Jimmy' ambaye ni meneja wa aliyekuwa msanii wa Bongo, Mzee Omar maarufu kama Mzee wa Mjegeje amefunguka kwamba chanzo cha kifo cha msanii huyo ni maradhi ya bandama na figo yaliyokuwa yakimsumbua.


Thabiti ameongeza kuwa, Mzee wa Mjegeje alitoa kauli kuwa akifa asizikwe nyumbani kwao Bagamoyo, badala yake azikwe Dar es Salaam kwa sababu ndugu zake wote walimkataa wakati akiugua.


"Mzee alikuwa anaumwa serious sana tukampeleka Hospitali ya Palestina (Sinza). Ameanza kuugua kama mwezi mmoja hivi uliopita akisumbuliwa na bandama na figo, miguu ilianza kuvimba.


"'Nilipambana kwa kadri navyoweza lakini kwa sababu sina kipato cha kutosha, tukawacheki ndugu zake, wakamkataa kipindi anaumwa. 


Mwanaye Shufaa anajua kila kitu kinachoendelea na nilikuwa nampa taarifa kila kitu kuhusu hali ya mzee.


"'Lakini leo kafariki, ndugu zake wanajitokeza wanataka mwili. Mimi niliweka rahani mpaka vitu vyangu ili mzee apate matibabu," amesema Thabiti.


Mzee wa Mjegeje aliyetamba kwenye mitandao ya kijamii kwa video yake ya "'Kata simu tupo site' amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Machi 20, 2024 katika Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala, Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu.


Thabiti amesema kuwa, Mzee wa Mjegeje alitoa kauli kuwa akifa asizikwe nyumbani kwao Bagamoyo, badala yake azikwe Dar es Salaam kwa sababu ndugu zake wote walimkataa enzi za uhai wake.


"Hatujafikia mwafaka wowote mpaka sasa, kwa sababu mimi na mama yangu ambaye ni mama Kipwasa (Mjumbe) lakini ndugu walimkataa kabisa.


"Mzee aliniambia kuna ndugu yake mmoja tu anaitwa Shaidi, huyo ndiyo utakaa naye kujua mimi nazikwa wapi lakini msinipeleke bagamoyo, nizikeni Dar es salaam kwa sababu ndugu zangu wote wamenikataa.


"Sasa leo wanakuja watu ambao siwajui, namjua mmoja ambaye nilisikia sauti na leo amekuja nikahakiki kuwa ni yeye.


"Mara ya mwisho nampa mzee uji saa saba kasoro uaiku alikuwa akiongea kwa tabu sana, nikamwambia utapona akaniambia Thabiti naomba msinipeleke Bagamoyo.


"Alitamka kauli kuwa ndugu zake wasihudhurie kwenye mazishi yake, hata wakinipeleka Bagamoyo mimi sitaenda nitakatagoma," amesema Thabiti.


Mzee wa Mjegeje alikuwa msanii kutoka Bagamoyo, Tanzania ambaye alikuwa akijihusisha na shughuli zote za sanaa hasa za maigizo ya vichekesho na uimbaji wa muziki.


"Kwa sababu ndugu zake hawataki kukaa na sisi, kuongea na sisi vizuri, wala kuelewana na sisi na wala hawana umoja na sisi, wanakuja kiubabe hawana ubinadamu, na sisi tutaenda nao kibabe. Kama mzee leo hatoki basi inshallah atazikwa hata kesho.


"Gharama zote za kutoa mwili na mambo mengine mpaka kumpumzisha mzee wetu ni kama Tsh laki saba hivi. Yeyote yule ambaye ameguswa na hili anaweza kutuchangia chochote tumpumzishe salama kwa Amani.


"Mpaka sasa hivi hakijapatikana chochote, ndiyo tunataka tukae kiko na Aunt Lulu na Mama yangu Mama Kipwasa ili tujadili tone tunafanya nini. Tangu akiwa hai alisema hana ndugu kwa sababu wao walimkana," amesema Thabiti.

No comments:

Post a Comment