Baada ya kukosolewa kusafiri nje ya nchi mara kwa mara, Rais wa Nigeria Bola Tinubu amepiga marufuku ya miezi mitatu kwa mawaziri na maafisa wengine wa serikali kwenda safari za nje zinazofadhiliwa na fedha za umma.
Afisa wa ngazi za juu amesema hatua hiyo baada ya Rais kuwa na wasiwasi wa kuhusu kupanda kwa gharama za safari kwa viongozi hao.
Marufuku hiyo itaanza kutekelezwa tarehe 1 Aprili.
Rais Tinubu na utawala wake wamekuwa wakikosolewa na baadhi ya watu kwa ziara zao za mara kwa mara nje ya nchi.
Tangu kuapishwa kwake mwezi Mei, Bw Tinubu amefanya zaidi ya safari 15 za kigeni.
Rais wa Nigeria anasemekana alitumia angalau naira 3.4bn (5,81,730,848TZS) kwa safari za ndani na nje katika miezi sita ya kwanza ya urais wake , ikiwa ni 36% zaidi ya kiasi kilichopangwa kwa 2023, gazeti la Punch la Nigeria liliripoti mwezi Januari.
No comments:
Post a Comment