Na Mwandishi Wetu, Dodoma
KATIBU wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Dodoma Mjini Isack Ngongi amewasisitiza viongozi wa chama ngazi ya kata kuhakikisha wanafanya vikao ili kukiimarisha chama na jumuiya zake.
Ngongi ameyasema hayo jijini Dodoma wakati akizungumza na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa kata ya Kikombo
Amesema uhai na uimara wa CCM ni vikao hivyo ni muhimu vifanyike mara kwa mara.
“Viongozi wa chama ngazi kata kuweni wakali hakikisheni watendaji wa jumuiya zote wanafanya vikao mara kwa mara kwasabau uhai wa CCM ni vikao kama kuna atakaye kaidi basi aandikiwe ripoti ili ipelekwe kweye ngazi za juu,”amesema
Ameongeza kuwa:”Lazima tuhamasishe vikao vifayike pamoja kusoma mapato na matumizi ili kuondoa sintofahamu kwasababu kila kitu kitakuwa wazi,”
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Kikombo Emmanueli Manyono alisema Rais Dk.Samia ameendelea kutoa fedha za kuendesha miradi mbalimbali ya maendeleo katika kata hiyo ikiwemo ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kilometa 16.
No comments:
Post a Comment