'UTOVU WA NIDHAMU' SABABU YA JOB KUACHWA TAIFA STARS- JEMEDARI SAID. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, March 14, 2024

'UTOVU WA NIDHAMU' SABABU YA JOB KUACHWA TAIFA STARS- JEMEDARI SAID.


Kocha wa Taifa Stars HEMEDI SULEIMAN MOROCCO ametaja wachezaji 23 watakaosafiri na Taifa Stars kwenda Azerbaijan bila jina la beki wa Yanga SC Dickson Job na kuzua maswali na ukosoaji kutokana na kiwango cha beki huyo kwa sasa pia ukweli kwamba alikuwamo kwenye kikosi cha wachezaji 27 waliocheza AFCON 2023 iliyofanyika 2024 Ivory Coast.


Sababu kubwa na ya msingi ya kuachwa Job iliyoandikwa na mchambuzi Jemedari Said ni utovu wa nidhamu na kukosa uzalendo kwa kitendo cha kukataa kucheza mechi dhidi ya Congo DR ambayo ilikuwa muhimu kwa Taifa Stars mchezo uliochezwa pale Korogho Ivory Coast.


Kocha Morocco aliyekuwa anakaimu ukocha wa Stars baada ya Amrouche kusimamishwa na CAF, alimpanga Job nafasi ya beki wa pembeni kulia (namba 2), kisha akaita kikosi kufanya nacho kikao kazi kabla ya mechi na kuelekeza mbinu za kuikabili DRC kwenye mchezo huo, baada ya kumaliza ndipo Job alinyoosha kidole akasema yeye hayuko tayari kucheza namba 2.


Ikabidi kocha ambadilishe na nafasi yake kupewa Lusajo Mwaikenda wa Azam ambaye alipambania Taifa mpaka mwisho. Inaelezwa nahodha wa Stars MBWANA Samatta aliongea na kocha kwamba angeongea na Job ili acheze lakini kocha akamwambia muache usimlazimishe. Mechi illisha kwa sare ya 0-0.


Job mara nyingi Yanga amekuwa akicheza kama beki wa kati amecheza mechi kadhaa na Stars akiwa kama beki wa pembeni (namba 2) mfano ni mechi dhidi ya Uganda pale Misri ambayo Stars ilishinda 1-0 bao la Msuva, eye Job alipiga krosi kwa Msuva akiwa pembeni kulia.


Mara kadhaa hasa wakati wa kocha Nabi tumeshuhudia Job akicheza kama namba 2, lakini siku hiyo alikataa katakata kitendo ambacho kimechukuliwa kama kukosa utayari wa kutumikia Taifa na kukosa uzalendo kwa chi tena ikiwa vitani kupambana na adui.


Job alipogundua kosa alirudi kuomba msamaha ndipo akaulizwa kama alipoumia Lusajo angeweza kuingia akajibu NDIYO, akaulizwa sasa kwanini ulikataa kucheza akakosa jibu.



Dickson Job ni kijana mdogo bado Taifa linamtegemea nadhani kwa hili anapaswa kuliomba radhi Taifa kwa kukosa uzalendo tumsamehe aendelee kutumika timu ya Taifa, vinginevyo tutakua hatumsaidii ila tunamjaza ujinga.

No comments:

Post a Comment