WAZIRI WA BIASHARA DKT. ASHATU KIJAJI KUFUNGUA SEMINA YA DCTS 28 MACHI 2024, DAR - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, March 19, 2024

WAZIRI WA BIASHARA DKT. ASHATU KIJAJI KUFUNGUA SEMINA YA DCTS 28 MACHI 2024, DAR


NA ANDREW CHALE.

WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa Semina maalum kuhusu Mpango wa Biashara wa nchi ya Uingereza na Nchi zinazoendelea (UK Developing Countries Trading Scheme – DCTS) itakayofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa jijini Dar es Salaam, tarehe 28 Machi 2024, kuanzia saa 3:00 asubuhi.


Kwa mujibu wa taarifa kwa umma iliyotolewa kwa Vyombo vya habari na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Semina hiyo ina lengo la kufahamisha wadau wa biashara nchini juu ya fursa ya mauzo ya bidhaa za Tanzania katika soko la Uingereza kupitia Mpango wa Serikali ya Uingereza wa Kufanya Biashara na Nchi zinazoendelea na inatarajiwa kufungwa na Mhe. Omar Said Shabaan, Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda, Zanzibar.

“Mpango wa DCTS ulizinduliwa Mei,2023, ambapo Tanzania ni miongoni mwa nchi 65 ambazo Uingereza imezijumuisha katika mpango huo ili kuweza kuuza bidhaa zake bila kulipa ushuru na imeingia pia katika kundi la nchi ambazo asilimia 99 ya bidhaa zake zitanufaika na msamaha wa kodi.


Lakimi pia, Semina hiyo ina lengo la kufahamisha wadau wa biashara nchini juu ya fursa ya mauzo ya bidhaa za Tanzania katika soko la Uingereza.” Imebainisha taarifa hiyo.


Walengwa wa semina hiyo ni wadau wa biashara wenye nia ya kuuza bidhaa za aina mbalimbali katika soko la Uingereza ambapo Wadau wanaweza pia kushiriki katika Semina hiyo kwa njia ya mtandao, kupitia link maalum ya mtandao wa “Teams” itakayotolewa kwa watakaojisajili kupitia:https://docs.google.com/forms/d/e/1FAIpQLSdjoGDLwkXfu9PWlV7Oc3LOnn5tRyELsimZVUaMaFhCGFB1Mw/viewform.
 

Aidha, imebainisha kuwa, Wananchi wote wanaweza kuifuatilia Semina hiyo kupitia na chaneli ya YouTube ya Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza ijulikanayo kama Ubalozi London (http://www.youtube.com/@ubaloziLondon).

No comments:

Post a Comment