Jeshi la Kenya lilifanya operesheni Alhamisi kuwaokoa wahanga wa mvua kubwa iliyosababisha vifo vya darzeni za watu kote Afrika Mashariki katika muda wa mwezi mmoja uliopita.
Takriban watu 45 wamekufa katika mafuriko nchini Kenya tangu mwezi Machi, ikiwa ni pamoja na 10 tangu Jumatatu, Shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya lilisema.
Sehemu kubwa za jiji kuu la Nairobi na miji mingine mikubwa zimefurika maji, hali inayowalazimu maelfu ya wakaazi kuondoka makwao.
Collins Obondo, mwenye umri wa miaka 38, alipoteza takriban jamaa wanne kwenye mafuriko Jumatano katika mtaa wa Mathare wenye wakazi wengi jijini Nairobi, ambao uko kando ya Mto Nairobi.
Rais wa Kenya William Ruto alisema katika mkutano na maafisa wakuu serikalini kwamba wanajeshi wanatumwa kusaidia shughuli za uokoaji. Naibu wake, Rigathi Gachagua, alisema kituo cha kukabiliana na dharura kilianzishwa Alhamisi.
Katika nchi jirani ya Tanzania, idadi ya vifo kutokana na mvua hiyo imefikia 155, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliliambia bunge Alhamisi.
Mamia kwa maelfu wamelazimika kukimbia makazi yao nchini Burundi. Wanasayansi wanasema mabadiliko ya hali ya hewa yanasababisha matukio ya hali ya hewa kali na ya mara kwa mara.
No comments:
Post a Comment