Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapiduzi (CCM) Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi amesisitiza dhamira ya Chama, chini ya Uongozi wa Mwenyekiti wa CCM, Dk. SAMIA Suluhu Hassan, ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kukirudisha kwa wanachama, kupitia kwa mabalozi, itatekelezwa kwa vitendo.
Akizungumza na viongozi wa CCM wa ngazi mbalimbali kuanzia mashina hadi mkoa, Mkoa wa Ruvuma, kwenye mkutano wa ndani uliofanyika Ukumbi wa Parokia ya Bombambili, mjini Songea, Aprili 20, 2024, Dk Nchimbi amesema kuwa kutambua ukubwa wa nafasi ya Balozi na Shina ni kutambua dhamana kubwa waliyonayo wanachama kwa Chama chao Cha CCM.
Aidha, Dk. Nchimbi pia amewapongeza na kuwashukuru wananchi na viongozi wa mkoa wa Ruvuma kwa mapokezi nakubwa yaliyoonesha imani kubwa waliyonayo kwa Chama Cha Mapinduzi.
Mkutano huo uliojumuisha Viongozi mbalimbali wa Chama , Serikali, Dini, Wazee na Taaasisi zisizo za kiserikali, Balozi Dkt. Nchimbi amewapongeza wana Ruvuma kwa kushinda chaguzi zote zilizopita siku za hivi karibuni hali inayozidi kuonesha imani yao kwa CCM haijatetereka na kutoa pongezi kwa ushirikiano wao mkubwa wa chama na serikali.
" _Hongereni kwa uhusiano mkubwa na mzuri wa chama na serikali na huu ndio unapelekea utekelezaji wa ilani kutekelezwa kwa kasi._ "
Aidha, Balozi Dkt. Nchimbi amehimiza juu ya heshima kwa mabalozi kwa kuwa ndio msingi imara wa CCM.
" _Nilipokuwa mbunge wenu hakuna watu ambao niliwapa heshima kubwa kama mabalozi ssbabu najua mabalozi ndio msingu wa shina la CCM na ndio maana tumeelekeza nguvu kubwa kuhakikisha Nchi nzima viongozi wote wanatambua hakuna viongozi wakubwa zaidi ya mabalozi na kwa mantiki hiyo chama kitarudi kwa wanachama wengine na sisi tunaochaguliwa na kuteuliwa ni watumishi tu kwa hao wanachama_ "
Katibu Mkuu wa CCM Balozi Dk Nchimbi, akiambatana na Katibu wa NEC ya CCM Taifa, Oganaizesheni, Ndugu Issa Haji Usi Gavu na Katibu wa NEC ya CCM Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Ndugu Amos Gabriel Makala, ameingia Mkoa wa Ruvuma Aprili 19, 2024, kwa ajili ya ziara yake katika maeneo mbalimbali mkoani humo, ikiwa ni mwendelezo wa ziara aliyoanzia mikoa ya Katavi, Rukwa, Songwe, Mbeya, Njombe na Ruvuma.
No comments:
Post a Comment