Na Carlos Claudio, Dodoma.
Waziri wa madini Mhe. Anthony Mavunde ametoa ahadi ya kufuta leseni za utafiti ambazo hazifanyiwi kazi ili kuepuka unyanyasaji wa wachimbaji wadogo unaowapelekea kuwa watumwa wa nchi yao.
Hayo yamesemwa jijini Dodoma kwenye mkutano wa kamati tendaji na halmashauri kuu ya FEMATA katika utiaji saini wa makubaliano ya ukodishaji na uuzaji vifaa vya uchimbaji wadogo kati ya STAMICO na META.
Amesema ni jukumu la serikali kuwaongoza wachimbaji wa madini katika njia sahihi za uchimbaji kupitia tafiti bila kujali gharama.
“Kilio chetu ni kwamba mnapoteza mitaji na nguvu nyingi sana kwa kuchimba na kubahatisha, hivyo serikali haiwezi kukwepa jukumu la kimsingi kabisa kupitia tafiti na baati mbaya sana tuliambiwa kiwa tafiti ni gharama,”
Mavunde amesema, “Kwa mwaka wa fedha uliopita, mchango wa sekta ya madini katika ukusanyaji umechangia bilioni 678 ya mchango wa wachimbaji wadogo.”
Amesema tarehe 1 mwezi wa 7 serikali inaenda kutekeleza mradi wa kupima eneo ka kilomita za mraba 165,655 sawa na asilimia 18% ya nchini Tanzania.
Kwa upande wake rais wa FEMATA Mhe. John Bina amesema FEMATA inaendelea kushirikiana na serikali kupitia tume ya madini ili kuhakikisha uchimbaji salama pamoja na kupatia wachimbaji wadogo vitambulisho.
Amesema malengo yao ni kuona wachimbaji wadogo wanapiga hatua kutoka wachimbaji wadogo kwenda hatua ya kati hadi wachimbaji wakubwa.
“Jina la FEMATA limepewa maono na Mhe. Rais wetu mama Samia Suluhu Hassan na kuiona Tanzania inanufaika na kampuni yetu kupitia kodi, FEMATA inaendelea kuwahamasisha wachimbaji wenzetu kuhusu umuhimu wa kulipa kodi na kuishahuri serikali TRA iwe inatoza kiwango cha 2% ya kodi ya mapato kwa wachimbaji wadogo kwa madini yote.”
Kwa upande wa mkurugenzi mtendaji wa STAMICO Dkt. Venance Mwasse amesema wapo bega kutengeneza ushirikiano baina ya wachimbaji na kuongeza ujuzi ambao mnufaika mkubwa atakuwa mchimbaji mdogo.
Nae Mhandisi Issa Mndeme kutoka kampuni ya META amesema wapo katika utiaji saini wa makubaliano ya ukodishaji na uuzaji vifaa vya uchimbaji wadogo katika kazi za madini huku kampuni yao ikijihusisha na usambazaji pamoja na kuuza vifaa vinavyotumika katika uchimbaji madini, ujenzi na kazi zinazohusisha mashine kubwa, amesema kampuni ya META ipo chini ya kampuni ya Meta Group Africa inayofanya kazi katika nchi 7 nchini Afrika ikiwemo Tanzania, Rwanda, Uganda, Kenya, Angola, Msumbiji na Zambia.
No comments:
Post a Comment