Mahakama ya Wilaya ya Hanang imemhukumu aliyekuwa Mkusanya Mapato kwa kutumia mashine ya POS wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang mkoani Manyara, Bw. PETRO MICHAEL MURAY.
Mshitakiwa ametiwa hatiani kwa kosa la ubadhirifu kosa ambalo ni kinyume na kifungu cha 28(1) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa sura ya 329 kama ilivyofanyiwa marejeo Mwaka 2022.
Hukumu hiyo dhidi ya Bw. Petro Michael Muray katika shauri la Uhujumu Uchumi Na.03/2023, imetolewa na Mhe. Anorld Kileo - Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Hanang - Aprili 19, 2024.
Mshtakiwa ameamriwa kwenda jela miaka 20 na ametakiwa kurejesha kiasi cha shilingi 3,532,000/= .
Mshitakiwa alifanya ubadhirifu wa fedha hizo kupitia makusanyo ya fedha kwa njia ya POS ambapo alikua akikusanya fedha zilizotokana na vyanzo vya misitu Wilaya ya Hanang.
Mshitakiwa amepelekwa magereza kutumikia kifungo chake.
No comments:
Post a Comment