Na Okuly Julius - Dodoma
Amesema dhana hiyo hairuhusu Mwanafunzi kurudishwa nyumbani kisa hajalipa michango mingine ikiwemo ya chakula ila uwepo utaratibu wa makubaliano ya wazazi na shule katika vikao vyao vya namna ya kuwabana wazazi au walezi ambao watashindwa kuwalipia watoto fedha ya chakula.
Prof. Mkenda ametoa kauli hiyo leo Aprili 5,2024 jijini Dodoma,wakati akifunga Mkutano wa Mwaka wa pamoja wa Tathmini ya Sekta ya Elimu kwa mwaka 2024.
“Elimu bila malipo haina maana kuwa ni elimu bure kwa sababu wazazi mnanunua madaftari na vitu vingine vya kumuwezesha mtoto kusoma bila changamoto sasa kwa sababu serikali ilishafanya kazi kubwa ya kutoa elimu bila malipo , jamii nayo ihamasike kuchangia baadhi ya michango ikiwemo chakula na isitokee mtoto akarudishwa nyumbani eti kisa hajalipa michango yeyote,” amesema Prof. Mkenda
Akizungumza juu ya mageuzi ya Elimu Prof. Mkenda amesema kuwa ni muhimu iwashirikishe wataalamu na wadau mbalimbali ili kuongeza ubora , kwani ndoto ya serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kuona matunda ya mageuzi hayo kwa vizazi vijavyo kwani sio ya kipindi kifupi ndio maana inahitaji umakini na ushirikishwaji wa kada mbalimbali.
No comments:
Post a Comment