SERIKALI YATATUA CHANGAMOTO YA UPATIKANAJI WA VITAMBULISHO VYA TAIFA (NIDA) - MASAUNI. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, April 15, 2024

SERIKALI YATATUA CHANGAMOTO YA UPATIKANAJI WA VITAMBULISHO VYA TAIFA (NIDA) - MASAUNI.



Na Okuly Julius, Dodoma

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Hamadi Masauni amesema ,
serikali imeiwezesha NIDA kumaliza tatizo la upatikanaji wa Vitambulisho vya Taifa kwa wananchi wa Tanzania Bara na Zanzibar lililokuwa kikwazo kwa wananchi katika kupata huduma mbalimbali za Kiuchumi na Kijamii.

Ameyasema hayo leo Aprili 15,2024 jijini Dodoma, wakati akizungumza na waandishi wa habari na kuelezea mafanikio ya miaka 60 ya Muungano wa Tanzania kwa Wizara hiyo na taasisi zake.


"Tunapoadhimisha miaka 60 ya Muungano tatizo hili linakwisha na kubaki historia, NIDA ilikuja na mpango mkakati wa uzalishaji mkubwa wa vitambulisho vya Taifa (Mass production) sambamba na ugawaji wa Vitambulisho kwa Umma (mass issuance) ulioanza kutekelezwa mwezi Oktoba 2023,

Na kuongeza " Mwaka 2008 Serikali iliidhinisha kuanzishwa kwa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) ambayo hadi sasa imefanikiwa kusajili watu 24,495,804, kutoa namba za utambulisho kwa watu 20,832,225 na kuzalisha vitambulisho 20,286,420.,"amesema Masauni


Masauni amesema , zoezi hilo la uzalishaji, usambaji na ugawaji wa Vitambulisho vya Taifa kwa umma linaendelea katika ofisi za Serikali za Mitaa, Vijiji, Vitongoji na Shehia ambako ndiko vitambulisho vinapelekwa kwa ajili ya wananchi kuvichukua.

Katika hatua nyingine Mhe. Masauni amesema katika kipindi cha Miaka 60 ya Muungano Idara ya Uhamiaji imeanza kutumia Mfumo wa Uhamiaji Mtandao unaounganisha Mifumo yote ya Utoaji huduma za kiuhamiaji kama vile Pasipoti, Visa, Vibali vya Ukaazi pamoja na Udhibiti na Usimamizi wa Mipaka kwa njia ya kielektroniki hali iliyoleta mageuzi makubwa ya kiutendaji.


Amesema uboreshaji wa mifumo ya utoaji Huduma za Uhamiaji Kidijitali zilianza kutekelezwa wakati wa Serikali ya Awamu ya Tatu ambapo Pasipoti zilianza kutolewa kwa kutumia Mfumo wa Kompyuta (zenye uwezo wa kusomeka kwa mashine), tofauti na awali ambapo Idara ilitoa Huduma hizo kwa njia ya kuandika kwa mkono, hali iliyosababisha ucheleweshaji wa huduma kwa wateja na kuongezeka kwa matukio ya kughushi nyaraka mbalimbali za Uhamiaji.


"Tangu kuzinduliwa kwa Mfumo wa Uhamiaji Mtandao mwaka 2018, Mfumo huu umeleta mageuzi makubwa ya kiutendaji katika Idara ya Uhamiaji. Mfumo huo unaunganisha Mifumo yote ya Utoaji huduma za kiuhamiaji kama vile Pasipoti, Visa, Vibali vya Ukaazi pamoja na Udhibiti na Usimamizi wa Mipaka kwa njia ya kielektroniki,"

Na kuongeza kuwa "mfumo umewezesha kubadilishana taarifa na mifumo mingine iliyo nje ya Idara yenye kutunza kumbukumbu mbalimbali za watu, kwa mfano Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Idara ya Kazi, RITA na Polisi,"amesema

Mfumo wa Uhamiaji Mtandao pia umesimikwa katika Vituo vya uwekezaji nchini (TIC) na Mamlaka Maalum ya Uzalishaji wa Mauzo ya Nje (EPZA) na Kituo cha Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) kwa lengo la kurahisisha upatikanaji wa Vibali vya Ukaazi kwa Wafanya biashara wa kigeni na wawekezaji.


Vilevile Idara ya Uhamiaji imefanikiwa kusimika mfumo wa kutolea Hati za safari za Dharura (ETD) za kieletroniki katika Wilaya 89 kati ya 91 zilizokusudiwa jambo ambalo limerahisisha utoaji wa huduma za kiuhamiaji katika wilaya 89 katii ya 91 zilizokusudiwa jambo ambalo limerahisha utoaji wa huduma za kiuhamiaji katika Wilaya hizi 89 pamoja na kuongeza ukusanyaji wa maduhuli ya Serikali.




No comments:

Post a Comment