SERIKALI YAWASHIKA MKONO WAATHIRIKA WA MAFURIKO KATA YA MHORO WILAYA YA RUFIJI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, April 11, 2024

SERIKALI YAWASHIKA MKONO WAATHIRIKA WA MAFURIKO KATA YA MHORO WILAYA YA RUFIJI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu nchi (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na wananchi wa kata ya Mohoro mara baada ya kukagua eneo ambalo limeathiriwa kwa mafuriko.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi akipanda mtumbwi wakati wa kukagua eneo ambalo limeathiriwa kwa mafuriko hayo.
Baadhi ya Mawaziri waliofika katika Kata ya Muhoro na kukagua eneo ambalo limeathiriwa kwa mafuriko hayo.
Baadhi ya Vikosi vya Uokoaji Kutoka Jeshi la zimamoto na Uokoaji waliopo katika kata ya Mohoro kwaajili ya kutoa msaada wa maokozi kwa wakazi walioathirika na mafuriko.
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

Na. Mwandishi Wetu Pwani

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama amewahakikishia waathirika wa Mafuriko Wilayani Rufiji Mkoani Pwani kuwa Serikali itagharamia huduma zote za msingi zinapatikana wakati wa kipindi hiki.

Ameyasema hayo tarehe 10 Aprili, 2024 wakati alipoongoza timu ya Mawaziri watano wa kisekta waliofika kushuhudia athari zilizotokana na Mafuriko katika eneo la Muhoro wilaya ya Rufiji Mkoani Pwani ambapo pia ametoa tahadhali kwa Wananchi katika maeneo yao kuhakikisha wanafuata maelekezo ya Wataalam na viongozi ili kuepukana na athari zitakazoweza kutokea wakati wa mvua zinapoendelea.

Waziri Mhagama amesema timu hiyo imefika katika eneo hilo ili kila Waziri  kuhakikisha eneo lake linasimamiwa ipasavyo kwa kutafuta mbinu mbadala za kuhakikisha waathirika hao wanapata huduma zinazostahili.

Aidha waziri Mhagama ametoa wito kwa uongozi wa wilaya ya Rufiji kuhakikisha chakula pamoja na mahitaji yanayopelekwa katika eneo hilo yatumike kwa walengwa na si vinginevyo.

"Kwenye huduma hizi za msingi ni pamoja na chakula, na  leo mmeondoka kwenye nyumba zenu na kitu kidogo cha kuwasaidia siku mbili tatu, mmemsikia Naibu waziri wa kilimo hapa tumeshaamua kwamba ni lazima chakula kiletwe cha kutosha na chakula kingine kiko njiani kitaingia leo na kesho, wito wangu mwingine ni kwa viongozi wa wilaya , chakula hiki kigaiwe kwa wahusika tu na si kunufaisha watu wengine ambao hawahusiki ,nitafuatilia na kuhakimisha kinawafikia waathirika." Alisema Mhagama.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Abubakar Kunenge amewataka wananchi kuendelea kuhama na kwenda katika  maeneo ambayo hayajaathirika na maji ili kuweza kupatiwa huduma zinazotolewa na Serikali.

"Tuangalie Maji maana  yanaendelea na mvua zinaongezeka kwa hiyo tuchukue tahadhali kadri maji yanavyoongezeka tusogee ,tusiseme tumezoea maji haya ni mafuriko yametokea mvua zimekuwa nyingi na nyingine sio za hapa lakin zinaingia katika mto yanajaa hapa, kubwa ni kwamba hakuna mtu atakayekufa kwa njaa hakuna atakae kosa huduma ya kiafya wala ya kuhifadhiwa na matibabu maana Serikali inawathamini sana." Alisema Kunenge.

No comments:

Post a Comment