TACAIDS ina andaa mkakati wa ukusanyaji raslimali fedha kwa ajili ya Mwitikio wa UKIMWI nchini - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, April 18, 2024

TACAIDS ina andaa mkakati wa ukusanyaji raslimali fedha kwa ajili ya Mwitikio wa UKIMWI nchini



Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) Dkt. Jerome Kamwela amewataka wadau kutoa ushirikiano kwa maoni na mawazo yao chanya ambayo yataboresho mkakati wa ukusanyaji fedha kwa ajili ya mwitikio wa UKIMWI nchini (HIV Sustainable Financing Framework) unaondaliwa na TACAIDS.

Mkakati huo unaandaliwa kwa ajili ya kuboresha njia za kukusanya rasilimali fedha zitakazosaidia utekelezaji wa shughuli za VVU na UKIMWI pamoja na utoaji wa huduma za UKIMWI kuwa endelevu hapa nchini, kwa kushirikisha wadau wa ndani ya nchini wakiwemo wadau kutoka kwenye sekta binafsi.

Akizungumza na washiriki katika kikao cha wadau cha kupitia rasimu ya mkakati huo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS Dkt Jerome Kamwela, amesema kuwa kuekelea 2030 ambapo Dunia inatarajia kumaliza UKIMWI suala la upatikanaji wa raslimali fedha kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli za UKIMWI pamoja na utoaji wa huduma za UKIMWI kutoka katika vyanzo vya ndani ya nchi ni la kupewa kipaumbele kikubwa.

“Hivi sasa suala la UKIMWI ni la kila mmoja wetu hapa nchini, hivyo ni muhimu kwa pamoja tukaangalia ni kwa namna gani tutashirikiana ili kupata raslimali fedha kwa ajili ya Mwitikio wa UKIMWI kutoka katika vyanzo vya ndani” alisema Dkt. Kamwela. 


Kuhusu hali ya UKIMWI nchini, Dkt Kamwela alifafanua kuwa utafiti uliozinduliwa tarehe 1 Disemba, 2023 ulionesha kwamba, watu elfu 60 wanapata maambukizi mapya kwa mwaka hapa nchini. Wakati matarajio ilikuwa ifikapo mwaka 2020 maambukizi mapya yawe chini ya watu elfu 20 kwa mwaka hapa nchini, hivyo bado kuna kazi kubwa ya kufanya kuhakikisha rasilimali fedha zinapatikana ili kupambana na UKIMWI hapa nchini. Aliongeza kuwa, mkakati huo utasaidia pia kuonesha maeneo ya kipaumbele yatakayoleta matokeo ya haraka. 

Dkt Kamwela ameongeza kuwa ili kufikia lengo la kumaliza UKIMWI ifikapo 2030 jitihada za mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI ikiwa ni pamoja na kubuni mbinu bora za utekelezaji wa afua za UKIMWI zinahitajika katika kuzuia maambukizi mapya na kumaliza vifo vitokanavyo na UKIMWI. 

Fedha nyingi bado zinahitajika katika utekelezaji wa shughuli za UKIMWI nchini ambapo kwa mwaka tunahitaji dola milioni 500 hadi 600. Hadi sasa asilimia 90 ya fedha kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli za UKIMWI nchini zinategemewa kutoka kwa wafadhili wa nje ya nchi wakati tatizo la UKIMWI letu.


Mwakilishi kutoka Mpango wa Taifa wa kudhibiti UKIMWI, Kifua kikuu na Magonjwa ya ngono - NASHCOP Dkt. Boniface Mlay ameshukuru jitihada zinazofanywa na TACAIDS ambaye ndiye mratibu wa shughuli za UKIMWI nchini na mwenye jukumu la kutafuta rasilimali kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli za UKIMWI pamoja na utoaji wa huduma za VVU na UKIMWI hapa nchini.

Dkt Boniface aliendelea kusema kwamba, fedha zinahitajika na asilimia 80 ya dawa na vifaa tiba vinaletwa na wafadhili, lakini uhitaji wa fedha bado ni mkubwa, na hivyo maoni ya kila mmoja hapa ni muhimu, ili kuhakikisha tunapata huu Mkakati na kuona ni namna gani tunapata vyanzo vya kudumu vya fedha za Mwitikio wa UKIMWI.

Akizungumza kwa niaba ya wadau wa maendeleo, Dkt. Mariam Ngaeje mtaalam wa haki ya afya ya uzazi na UKIMWI kutoka UNFPA amesema wadau wa maendeleo wanaendelea kuunga mkono na kutoa michango ya fedha na utaalam katika jitihada ambazo zinafanywa na serikali katika mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI na kufika malengo yaliyowekwa ya kumaliza UKIMWI ifikapo 20230

Wote tunalenga katika kuhakikisha kwamba hatuna maambukizi mapya kama nchi na watu hawapati changamoto zinazoendana na upungufu wa kinga mwilini pamoja na vifo ifikapo 2030

Dkt Marim ameishukuru serikali kwa jitihada zinazofanywa za kupata rasilimali fedha kutoka vyanzo vya ndani ili kufanikisha kila mtanzania anakuwa na afya njema na ustawi bora. ni kweli kuwa jitihada za serikali ni kwa ushirikiano na wadau wa maendeleo ikiwemo mashirika ya kimataifa. Tunajitahidi kuchangia kwenye kile ambacho serikali inakifanya kuhakikisha tunakuwa na fedha za ndani kwa ajili ya mwitikio wa UKIMWI.

 “tunategemea maarifa na uzoefu wenu vitatusaidia kuboresha mkakati huu na kupata vyanzo endelevu kwa ajili ya upatikanaji wa fedha za mwitikio wa UKIMWI, ikiwa ni pamoja na namna bora kushirikisha sekta binafsi katika kuchangia utekelezaji wa shughuli za UKIMWI nchini pamoja na utoaji huduma bora za VVU na UKIMWI nchini.” 

No comments:

Post a Comment