WAKURUGENZI WA BODI YA REA WARIDHISHWA NA UTENDAJI WA MENEJIMENTI YA REA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, April 30, 2024

WAKURUGENZI WA BODI YA REA WARIDHISHWA NA UTENDAJI WA MENEJIMENTI YA REA


Bodi ya wakurugenzi  wa Nishati Vijijini REA  imeridhishwa na hatua mbalimbali za utekezaji wa maagizo yao kwa watendaji wa taasisi hiyo ikiwemo wa kufikisha umeme vijijini  huku wakishauri elimu Zaidi itolewe kwa wananchi umuhimu wa Nishati ya Umeme inayopolekwa vijijini ili waweze kuitumia katika kujipanua kichumi .


Wakurugenzi wa Bodi ya Nishati Vijijini wamegawana katika maeneo mbalimbali hapa nchi kuangalia utekelezaji wa maagizo ya bodi hiyo katika kufikisha umeme vijiji ambapo Kwa mkoa wa Manyara na Arusha wakurugenzi watatu wa Bodi STEVEN MWAKIFAMBA, 

SOPHIA MGONJA na RADHIYA MSUYA  walitembelea mikoa hiyo na kuridhishwa na utekerezaji wa miradi ya REA.

Wakiongea na waandishi wa habari Mkurugenzi wa bodi ya Nishati STEVEN MWAKIFAMBA  amewataka wananchi wanaoishi vijiji vilivyofikishiwa umeme kuunganisha katika nyumba zao  na maeneo ya biashara Kama malengo ya serikali yalivyokusudiwa.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa  bodi ya Nishati SOPHIA MGONJA amezitaka Taasisi ya REA na TANESCO kutoka elimu Kwa wananchi umuhimu wa kuunganisha umeme katika nyumba zao na maeneo ya kibiashara na kutumia umeme huo kujiingizia kipato

Naye mkurugenzi wa bodi ya nishati Radhia msuya ameseita menejimenti ya REA kuendelea kutoa kipaumbele kwenye maeneo ya huduma za kijamii ikiwemo shule,zahanati na ofisi za vijiji  pindi umeme unapofikishwa  vijijini ili kuongea ufanisi katika utendaji Kazi.



 Wakiwa mkoani manyara wilaya ya mbulu bodi ya wakurugenzi ya nishati ilikuta a na mkuu WA wilaya ya mbulu veronica Jessy Ambae alisema kufikisha umeme maeneo ya vijiji  ni mafanikio ya utekelezaji WA Iran ya CCM katika kuwahudunia wananchi wote ikiwemo walio vijijini.

Nao wananchi waliofaidika na kufikiwa na umeme kupiti wakala WA Nishati Vijijini REA wameaidi kutumia umeme Kwa kuwasha taa za nyumba zao lakini pia kuhakikisha unawasaidia kiuchumi katika kujiongezea kipato.

No comments:

Post a Comment