Wanaanga wa NASA wanajaribu kupanda mimea mwezini, katika mpango mpya ambao umeanza kutekelezwa.
Ujumbe wa NASA wa Artemis 3 kwenda mwezini umeweka lengo la 2026 la utekelezaji wa mpango huu.
Kwa sasa, wanasayansi wanataka kuelewa jinsi mwezi unaundwa na mabadiliko yanayotokea ndani yake, kutathmini ikiwa mwanadamu anaweza kuishi mwezini.
Sasa, NASA imetangaza kuwa itafanya tafiti tatu wakati wanaanga hao watakafanya safari yao ijayo ya mwezini.
Sehemu ya utafiti huu imedhamiria kuchunguza jinsi mwezi unavyosonga, ikiwa kuna matetemeko ya ardhi, ikiwa maji au barafu inaweza kupatikana kwenye ardhi ya mwezi na pia cha muhimu zaidi ni kwamba kuna mimea juu ya mwezi, na inaweza pia kukua vizuri.
No comments:
Post a Comment