OR-TAMISEMI
Mkurugenzi wa Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe Ofisi ya Rais – TAMISEMI Dkt. Rashid Mfaume amekemea watumishi wa sekta ya Afya wanaotengeneza taarifa uongo za wateja katika cliniki ya huduma na kinga (CTC) kwa watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi.
Dkt. Mfaume ametoa maelekezo hayo baada ya kukagua shughuli za uendeshaji na usimamizi wa shughuli za Afya katika kituo cha Afya Buzuruga wilaya ya Ilemela mkoa wa Mwanza akiwa ameambatana na timu ya Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe kutoka Ofisi ya Rais – TAMISEMI na amesema baadhi ya watumishi wa umma wanashirikiana na taarifa za udanganyifu wa takwimu kwa Kumekuwa na wateja wetu ambao wamekuwa wakihudhuria na kupata huduma ya matibabu kwenye cliniki yetu ya CTC
"Sisi kama ofisi tumeombwa na wadau wanaotoa fedha kwa namna gani kwa pamoja tunakabiliana na ubora wa takwimu kama linapungua liwe wazi kwamba kweli amefariki au amebadilisha makazi lakini pamoja na hizo ‘factors’ kuhama makazi na kufariki lakini kuna watumishi wenzetu ambao sio waaminifu walikuwa wanatoa takwimu ambazo sio sahii kwa maslahi ambayo wanaijuwa wao kwa hilo nielekeze kwa mikoa yote mkome,” amesema Dkt. Mfaume.
No comments:
Post a Comment