WAZIRI BASHE AIGAZI BODI YA KAHAWA KUONGEZA UZALISHAJI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, April 16, 2024

WAZIRI BASHE AIGAZI BODI YA KAHAWA KUONGEZA UZALISHAJI


Na Okuly Julius , Dodoma

WAZIRI wa Kilimo Hussein Bashe ameielekeza Bodi ya Kahawa Tanzania kuongeza uzalishashi wa kahawa kutoka tani 80,000 inayozalishwa sasa hadi kufikia tani 300,000 ifikapo msimu wa mwaka 2025/2026.

Bashe ameyasema hayo leo Aprili16,2024 jijiniDodoma, wakati akifungua mkutano mkuu wa 14 wa wadau wa kahawa wa mwaka 2024.


“Viongozi wa bosi nitawapima kwa kufikia lengo abalo mmejiwekea kufikisha tani 300,000 ifikapo waka 2025/2026. Hakuna sababu ya kushindwa kwasababu serikali imeweka mazingira wezeshi kwa wakulima ikiwemo kusambaza miche ya kahawa kwa wakulima.

Aliongeza kuwa:” Haya ni maelekezo ambayo yatawekwa kwa maandishi ili hata atakayekuja ataendeleza pale tulipoishia. Tunataka za la kahawa liinuke na kuwafaidisha wakulima wadogo kwani ndio lendo la serikali inayoongozwa na Rais Dk.Samia Suluhu Hassan.


Katika hatua nyingine Bashe alisema hali ya utumiaji wa kahawa kwa wananchi bado iko chini ambapo ni asilimia saba.

Aliiagiza bodi hiyo kuhakikisha inaenelea kuhamasisha wananchi kutumia kahawa ili kuhakikisha kunakuwa na masoko ya ndani hakikika kwa wakulia wa zao hilo.
“Kwasasa mwamko kwa Watanzania kutumia kahawa bado iko chini ambapo takwimu zinaonyesha ni asilimia saba tu. Bodi ina kazi ya uhakikisha inaandaa matamasha mbalimbali kwa ajili ya kuhamasisha watanzania kutumia kahawa ambapo itasaidia kuongeza uhakika wa masoko ya ndani kwa wakulia,”alisema


Mwenyekiti wa Bodi ya Kahawa Prof. Aurelia Kamuzora, alisema malengo ni kuzalisha tani 300,000 za kahawa ifikapo mwaka 2025 kutoka tani 80 za hivi sasa.


Pia, Prof. Kamuzora amewataka wakulima wa kahawa nchini kutumia mfumo rasmi wa uuzaji zao hilo na kujipesha na walanguzi ambao wamekuwa wakiwadanya kuuza kwa bei ya hasara.


Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge Viwanda,Bisahara,Kilimo na Mifugo Mariam Ditopile, alisema wataendelea kuisimamia serikali kutenga bajeti ya kutosha katika sekta ya Kilimo.


Ditopile, amesema ipo haja ya kuwekeza katika soko la ndani na kahawa ili kuwa na uhakika kwa wakulima tofauti na ilivyo sasa ambapo kiasi kinachouzwa nje kinaongezwa thamani na kurudi nchini kwa bei ya juu.



No comments:

Post a Comment