Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amekutana na kuzungumza na Wabia wa Maendeleo (Development Partnerd Working Group) kujadili namna bora ya kuendelea kuwezesha Makandarasi na Washauri Elekezi Wazawa kushiriki katika miradi ya ujenzi wa miundombinu ya barabara na madaraja ambayo inaendelea kutekelezwa na Serikali.
Kikao hicho kimefanyika leo Mei 21, 2024 jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Wabia wa Maendeleo, Viongozi na Watendajii Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Ujenzi wakiongozwa na Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Ujenzi, Mhandisi Aloyce Matei.
Waziri Bashungwa amewashukuru Wabia wa Maendeleo kwa kuendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kufadhili utekelezaji wa miradi mbalimbali ya miundombinu ya barabara, madaraja na uboreshaji wa viwanja vya ndege hapa nchini unaoendelea.
Aidha, Bashungwa amesisitiza umuhimu wa Wabia wa Maendeleo kufadhili miradi ya ujenzi itakayotekelezwa na Wakandarasi na Washauri Elekezi Wazawa hapa nchini ikiwemo ukuaji wa uchumi kwa jamii na Taifa kiujumla.
No comments:
Post a Comment