Hospitali ya Rufaa Kanda Mbeya, imeendelea kushiriki katika kukuza na kuimarisha ubora wa huduma za afya nchini na kitovu cha huduma za afya katika Nyanda za Juu Kusini kuwa na madaktari bingwa na bobezi kwa kushiriki katika utekelezaji wa huduma za kibingwa za Mkoba zinazotolewa na kambi ya Madaktari bingwa wa Dkt. Samia katika kuwahudumia wananchi katika mikoa mbalimbali.
Timu ya Viongozi na Wataalamu kutoka Kituo cha afya cha Mt. Theresia Wenda Iringa vijijini ikiongozwa na Mganga Mfawidhi na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Ndani Sr. Dkt. Sabina Mangi, wamefanya ziara ya siku moja katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya kwa lengo la kujionea na kujifunza mambo mbalimbali ya utoaji huduma na pia kuanzisha ushirikiano na Hospitali ya Rufaa ya kanda Mbeya kwaajili ya kuwajengea uwezo watumishi wa kituo hicho cha afya.
Sista Mangi ameeleza kuwa msukumo huwo wa kuitembelea Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya umetokanana na Madakati bingwa na bobezi kutoka hospitali ya kanda Mbeya waliokua wakitoa huduma Mkoba katika kambi ya Madaktari bingwa wa Dkt. Samia katika kituo hicho kuonekana ni watumishi ambao kwa namna wanavyofanya kazi zao kwa furaha, ukamilifu na kwa taaluma hivyo, wakaona ni vyema kuja kujifunza kutoka na ufanisi huo mkubwa walioonyesha
“Tumefika hapa tumeona kweli ni hospitali ambayo watumishi wake wanaonekana ni wanafuraha, wanaonekana wananmwamko, wanaonyesha ownership ya hospitali,na Mkurugenzi ametupokea vizuri akatueleza siri za mafanikio hayo na jinsi wanavyofanya kazi kwa ushirikiano mkubwa na watumishi. ” – Sr. Mangi
Amesema kupitia ziara hiyo kuwa wamejifunza mambo mnegi ikiwemo kufanya kazi kama timu na ushirikiano, maswala ya ubora kwa utekelezaji wa 5s KAIZEN na ushirikiano mkubwa kati ya Uongozi na watumishi kwa kuishi kama familia na kwa pamoja.
Sr. Mangi ameeleza kuwa na dhamira ya kushirikia na Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya katika kuwa na huduma mkoba pia kuanzisha programu ya kubadilishana wataalamu kwenda kituo cha afya cha Mt. Theresia na wengine kuja MZRH kwa lengo la kujengewa uwezo na kujifunza
“Tunataka kufanye kazi na ushirikiano na Hospitali ya Rufaa ya kanda Mbeya kwa kuwa na huduma mkoba kila baada ya miezi 3, pili kwapata watumishi watakaokuja kufanya kazi pamoja na sisi kwaajili ya kuwajengea uwezo watumishi wa kituo chetu, tatu kuwaleta watumishi wetu hospitali ya rufaa ya kanda Mbeya kwaajili ya kujifunza na kujengewa uwezo ili wakirudi waje watujengee uwezo wale hatukupata nafasi ya kuja huku”. – Sr. Mangi
No comments:
Post a Comment