NACTVET WAKUTANISHA WADAU WA ELIMU ZAIDI YA 260 DODOMA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, May 9, 2024

NACTVET WAKUTANISHA WADAU WA ELIMU ZAIDI YA 260 DODOMA


Na Okuly Julius, Dodoma

Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET), Dkt. Adolf Rutayuga,leo tarehe 9 Mei,2024, jijini Dodoma, amefungua rasmi kikao cha wadau, kinachojumuisha Wakuu wa vyuo na maafisa udahili ambao jumla yao ni 267, kinachojadili masuala ya udahili na upimaji, ili kubaini dosari zinazojitokeza wakati wa udahili ili kuzipatia ufumbuzi wa pamoja kwa manufaa ya wadau.

Dkt. Rutayuga amebainisha kwamba wakuu wa vyuo vya serikali na binafsi wameshirikishwa kwa kutambua nafasi zao kama watoa maamuzi na wakuzaji wa elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi.

Amewaasa wakuu wa vyuo kuwa na ufuatiliaji wa karibu wa maafisa udahili ili kuhakikisha wanavyuo wapya wanadahiliwa kwa kuzingatia vigezo,kanuni na miongozo inayotolewa na mara kwa mara ili kuhakikisha wahitimu wa vyuo nchini wanaoingia kwenye soko la ajira wakiwa na wamekidhi viwango vya ushindaji wa soko.


Wakati huo huo, Mkurugenzi wa Udahili, Utahini na Utunuku wa NACTVET, Dkt. Marcelina Baitilwake, amesema warsha hiyo ni ya muhimu sana kwa vyuo na wadau wote kwani changamoto ,ote zinajadiliwa kwa uwazi na kupatiwa suluhu ya pamoja.


Kwa upande wake, Meneja wa Udahili wa NACTVET, bi. Amina Aziz amezungumzia wajibu wa maafisa udahili katika mchakato mzima wa upatikanaji wahitimu wenye sifa.

Warsha hiyo iliwalenga wakuu wa vyuo na maafisa udahili katika vyuo vonavyotoa mafunzo ya afya na sayansi shirikishi (HAS), nchini.


No comments:

Post a Comment