Ebrahim Raisi alifikia karibu na kilele cha madaraka katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na alipigiwa upatu sana kupanda juu kabisa kwenye uongozi wa ngazi ya juu.
Amepatwa na hali ya ghafla ambayo haikutarajiwa.
Kifo chake katika ajali ya helikopta siku ya Jumapili kimechochea uvumi unaoongezeka juu ya nani hatimaye atachukua nafasi ya Kiongozi Mkuu wa miaka 85, Ayatollah Ali Khamenei, ambaye afya yake imekuwa jambo la kuzingatiwa kwa muda mrefu.
Hatima mbaya ya rais wa Iran mwenye misimamo mikali haitarajiwi kuvuruga mwelekeo wa sera ya Iran au kuitikisa Jamhuri ya Kiislamu kwa njia yoyote ile.
Lakini itajaribu mfumo ambapo watu wenye msimamo mkali wa kihafidhina sasa wanatawala matawi yote ya mamlaka, waliochaguliwa na ambao hawajachaguliwa.
"Mfumo huo utafanya maonyesho makubwa ya kifo chake na kushikamana na taratibu za kikatiba ili kuonyesha utendakazi, wakati unatafuta mwajiri mpya ambaye anaweza kudumisha umoja wa kihafidhina na uaminifu kwa Khamenei," anasema Dk Sanam Vakil, mkurugenzi wa Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini katika taasisi ya Chatam House.
Wapinzani wa Raisi watapongeza kuondoka kwa mwendesha mashtaka wa zamani anayeshutumiwa kwa jukumu muhimu katika mauaji ya halaiki ya wafungwa wa kisiasa katika miaka ya 1980, mauaji ambayo alikanusha; watatumaini mwisho wa utawala wake utaharakisha mwisho wa utawala huu.
Kwa wahafidhina watawala wa Iran, mazishi ya serikali yatakuwa tukio lililojaa hisia; pia itakuwa fursa ya kuanza kutuma ishara zao za mwendelezo.
Wanajua ulimwengu unatazama.
"Kwa miaka 40, katika simulizi za Magharibi, Iran ilipaswa kuanguka na kusambaratika," Profesa Mohammed Marandi wa Chuo Kikuu cha Tehran aliiambia BBC.
"Lakini kwa njia fulani, kimiujiza, bado iko hapa na ninatabiri bado itakuwa hapa katika miaka ijayo."
Nafasi nyingine muhimu ambayo lazima ijazwe ni kiti kinachoshikiliwa na kasisi huyu wa ngazi ya kati kwenye Bunge la Wataalamu, chombo kilichopewa mamlaka ya kumchagua kiongozi mkuu mpya, wakati mabadiliko hayo muhimu zaidi yatakapokuja.
"Raisi alikuwa mrithi anayetarajiwa kwa sababu, kama Khamenei mwenyewe alipokuwa kiongozi mkuu, alikuwa mchanga, mwaminifu sana, mwenye itikadi ya kujitolea kwa mfumo ambaye ana utambuzi wa majina," anasema Dk Vakil anayehusika na mchakato huu usio wazi wa uteuzi.
Majina yanayoonekana kuwa katika kinyang'anyiro hicho ni pamoja na mtoto wa Kiongozi Mkuu Mojtaba Khamenei.
Hata kabla ya kifo cha Raisi kuthibitishwa rasmi, Ayatollah alitangaza katika chapisho la X kwamba "Watu wa Iran hawapaswi kuwa na wasiwasi, hakutakuwa na usumbufu katika masuala ya nchi."
Changamoto ya haraka zaidi ya kisiasa itakuwa kuandaa uchaguzi wa mapema wa rais.
Madaraka yamehamishiwa kwa Makamu wa Rais Mohammad Mokhber; uchaguzi mpya lazima ufanyike ndani ya siku 50.
Wito huu kwa wapiga kura ulikuja miezi michache tu baada ya uchaguzi wa wabunge wa Machi kufichua idadi ndogo ya waliojitokeza kupiga kura katika nchi ambayo ilijivunia kushiriki kwa shauku katika zoezi hili.
Uchaguzi wa hivi majuzi, ikiwa ni pamoja na ule wa mwaka wa 2021 ambao ulimuweka madarakani Raisi kwenye kiti cha urais, piauligubikwa na kutengwa kwa utaratibu wa wapinzani wa wastani na wanaounga mkono mageuzi na bodi ya uangalizi.
"Uchaguzi wa mapema wa rais unaweza kumpa Khamenei na taasisi za juu za nchi fursa ya kubadili mwelekeo huo ili kuwapa wapiga kura njia ya kurejea katika mchakato wa kisiasa," anasema Mohammad Ali Shabani, mhariri wa tovuti ya habari yenye makao yake makuu London ya Amwaj.media.
"Lakini, kwa bahati mbaya, hadi sasa hatujaona dalili za serikali kuwa tayari kuchukua hatua kama hiyo."
Lakini, hata ndani ya safu ya Raisi, inaonekana hakuna mrithi dhahiri.
"Kuna kambi tofauti ndani ya kundi hili la wahafidhina, ikiwa ni pamoja na watu wenye msimamo mkali zaidi na wengine wanaochukuliwa kuwa waaminifu zaidi," asema Hamidreza Azizi, wa taasisi ya wasomi yenye makao yake makuu mjini Berlin.
Anaamini kuwa hii itaongeza ushindani wa sasa wa kugombea nafasi ndani ya bunge jipya na katika ngazi za mitaa.
Yeyote anayechukua vazi la Raisi anarithi ajenda ya udhibiti wa ukomo wa mamlaka.
Mamlaka ya mwisho ya kufanya maamuzi katika Jamhuri ya Kiislamu yako kwa Kiongozi Mkuu.
Sera ya kigeni, hasa katika eneo, ni Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) ambao wana nguvu zinazoongezeka.
Rais hakupiga risasi miezi kadhaa iliyopita wakati Iran ilipokabiliana na mvutano mkubwa na adui yake mkuu Israel juu ya vita vya Israel Gaza.
Ilianzisha sauti ya hatari na kuweka tahadhari katika miji mikuu mingi, zaidi ya yote Tehran, juu ya uwezekano wa kuongezeka kwa hatari zaidi.
Lakini alipokuwa akiendelea na uongozi wake wa kila siku, Wairani walijitahidi kukabiliana na matatizo ya kifedha yanayozidi kuhusishwa na vikwazo vya kimataifa pamoja na usimamizi mbovu na ufisadi.
Mfumuko wa bei ulipanda hadi zaidi ya 40%; sarafu ya rial ilishuka thamani.
Jamhuri ya Kiislamu pia ilitikiswa na wimbi la maandamano ya ajabu yaliyosababishwa na kifo cha Mahsa Amini mwenye umri wa miaka 22 Septemba 2022 ambaye alizuiliwa na polisi wa maadili kwa madai ya kukiuka kanuni kali za mavazi za Iran.
Wiki kadhaa kabla ya machafuko hayo, Raisi aliamuru kuimarishwa kwa "sheria ya hijabu na usafi wa kimwili" ya Iran ambayo inawajibisha wanawake kuwa na tabia na mavazi ya heshima ikiwa ni pamoja na kuvaa hijabu.
Lakini maandamano yaliyoongozwa na kizazi cha vijana wa kike, wakipinga safu ya vikwazo vilivyowekwa dhidi ya maisha yao, hasa yalilenga hasira yao kwenye vyanzo halisi vya mamlaka, Kiongozi Mkuu na mfumo wenyewe.
Mashirika ya kutetea haki za binadamu yanasema mamia waliuawa katika ukandamizaji huo na maelfu kuzuiliwa.
"Baada ya kuchaguliwa kwa idadi ndogo zaidi ya waliojitokeza kupiga kura katika uchaguzi wa rais katika historia ya Irani, Raisi hakuwa na mamlaka maarufu ya mtangulizi wake Rouhani," anasema Shabani akimzungumzia kiongozi wa mageuzi Hassan Rouhani ambaye umaarufu wake wa awali ulichochewa na makubaliano nyuklia ya 2015, ambayo yalisambaratika wakati Rais Trump alipoiondoa Marekani kwenye mkataba huo kikamilifu miaka mitatu baadaye.
Mazungumzo ya moja kwa moja kati ya utawala wa Rais Biden na timu ya Raisi yalipata mafanikio machache.
"Aliepuka hasira nyingi ambazo zilielekezwa kwa Rouhani na wapinzani wa Jamhuri ya Kiislamu, kwa kiasi fulani kwa sababu alionekana kuwa na ushawishi mdogo na asiyefaa," anaelezea Shabani.
Ajali hiyo pia ilimuua Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Hossein Amir-Abdollahian. |
Ajali hiyo ya helikopta pia iligharimu maisha ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Hossein Amir-Abdollahian ambaye alichukua jukumu kubwa katika kujaribu kuwasilisha kesi ya Tehran kwa walimwengu na kutafuta njia za kupunguza athari za adhabu za vikwazo.
Wakati wa diplomasia ya dharura kuzunguka vita vya Israel na Gaza, alikuwa sauti kwenye simu na uso katika mikutano na washirika wa Iran, pamoja na mawaziri wa mambo ya nje wa Kiarabu na Magharibi waliokuwa na wasiwasi wa kutuliza na kudhibiti mivutano.
"Alikuwa njia muhimu ya kupitisha ujumbe," kilisema chanzo kikuu cha kidiplomasia cha Magharibi. "Lakini ilionekana kuwa ya kimfumo kwani mamlaka hayakuwa katika wizara ya mambo ya nje."
"Kifo cha ghafla cha rais kwa kawaida ni tukio la matokeo lakini, licha ya kuonekana kama Kiongozi Mkuu anayetarajiwa, alikosa uungwaji mkono wa kisiasa na maono yoyote ya wazi ya kisiasa," anasisitiza mchambuzi Esfandyar Batmanghelidj, Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi za sera za Bourse and Bazaar . "Lakini watendaji wa kisiasa waliomchagua watarekebisha na kusonga mbele bila yeye."
No comments:
Post a Comment