OSHA WAENDESHA MAFUNZO YA USALAMA MAHALA PA KAZI KWA WAANDISHI WA HABARI DODOMA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, May 22, 2024

OSHA WAENDESHA MAFUNZO YA USALAMA MAHALA PA KAZI KWA WAANDISHI WA HABARI DODOMA


Na Okuly Julius, Dodoma

WAKALA wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) umesema utaendelea kuimarishaji mifumo ya usalama na afya kazini ili kuwafanya wawekezaji wajisikie fahari kuwekeza nchini lengo ni kuunga mkono jitihada za Rais Dk.Samia Suluhu Hassan.

Hayo yamebainishwa leo Mei 22,2024 jijini Dodoma na Mtendaji Mkuu wa OSHA Khadija Mwenda wakati akifunga mafunzo ya siku moja kwa waandishi wa habari kuhusu kuhusu usalama mahala pa kazi.

Amesema Rais Dk Samia amekuwa akiweka msisitizo mkubwa katika kuboresha mazingira ya uwekezaji na ufanyaji biashara nchini.

“Serikali ya Awamu ya Sita Chini ya uongozi wa Rais Dk.Samia unasisitiza mazingira rafiki ya uwekezaji katika kuunga mkono jitihada hizo OSHA tumekuwa tukiangalia ni namna gani tunaweza kuweka mazingira ambayo yatakuwa rafiki kwa uwekezaji na ufanyaji biashara yatakayowafanya wawekezaji kujisikia fahari kuwekeza nchini,”amesema.

Katika hatua nyingine Mwenda amesisitiza kuwa Rais Dk.Samia ameonyesha dhamira ya kuiboresha OSHA ili iweze kutimiza majukumu yake kwa ufasaha na ufanisi.

Amesema katika kuhakikisha hilo tayari serikali ya Awamu ya Sita imetoa magari 13,kibali cha kuajiri watumishi 44 na vifaa vya kisasa.

“Tunamshukuru Rais Dk.Samia kwa sababu ameonyesha dhamira yake ya kuiboresha OSHA na sasa tunaona ametoa fedha kwa ajili ya kununua vifaa vya kisasa vitakavyo saidia katika kutekeleza majukumu yetu. Na sisi tunawahakikishia kuwa tutaendelea kufanya kazi kwa weredi ili tuendelee kuunga mkono jitihda hizo,”amesema

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama Cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Dodoma (DPC) Mussa Yusuph amesema mafunzo hayo ni muhimu kwa wanahabari kwasababu wamekuwa wakifanya kazi katika mazingira hatarishi.

Amesema miongoni mwa vihatarishi vinavyo wakumba waandishi wa habari nchini ni kihatarishi cha kisaikolojia ambapo wengi wamekuwa wakifanya kazi bila kuwa na uhakika wa ujira, mazingira yasiyokuwa salama katika maeneo yao ya kazi, unyanyasaji wa kijinsia na malengo makubwa ya kazi kuliko uwezo uliopo.

“Kihatarishi kingine ni cha kiegonomia ambapo waandishi wamekuwa wakitekeleza majukumu yao kwa kutumia vifaa visivyozingatia usalama wao wa kiafya, kusimama muda mrefu pamoja na mtindo mbaya wa ufanyajikazi,” ameeleza.

Naye Mkufunzi wa huduma ya Kwanza OSHA Moteswa Meda, amesema huduma ya kwanza ni muhimu pindi watu wanapopata majanga wanapokuwa kazini kabla ya kufikishwa katika vituo vya kutolea huduma ya afya.

No comments:

Post a Comment