Marcus Rashford (kushoto) na Jordan Henderson wamekuwa tegemeo katika kikosi cha England kwa miaka mingi |
Marcus Rashford na Jordan Henderson wameachwa nje ya kikosi cha muda cha wachezaji 33 cha England kilichoteuliwa na kocha Gareth Southgate kwa ajili ya michuano ya Euro 2024.
Rashford, 26, mshambuliaji wa klabu ya Manchester United amekuwa na wakati mgumu katika kuwa na kiwango kizuri msimu huu, akifunga mabao saba na kusimamia mabao mawili katika mechi 33 za ligi.
Rashford alicheza katika mechi saba za England msimu huu kabla ya kuachwa nje dhidi ya Ubelgiji mwezi Machi, na sasa ameondolewa kwenye kikosi cha mazoezi cha Southgate.
Henderson alijiunga na Al-Ettifaq ya Saudi Arabia akitokea Liverpool majira ya kiangazi mwaka jana lakini aliwaacha na kujiunga na Ajax ambayo ilikuwa na matatizo mwezi Januari.
Southgate aliendelea kumjumuisha katika timu ya taifa baada ya kuhamia ligi kuu ya Saudia, ingawa alizomewa na baadhi ya mashabiki wa England kwenye mchezo wake wa kwanza kurejea nchini, dhidi ya Australia katika uwanja wa Wembley mwezi Oktoba, jambo ambalo meneja huyo wa Uingereza alisema wakati huo "halikuwa na msingi".
Henderson alikuwepo kwenye kikosi kilichocheza mechi za kirafiki mwezi Machi dhidi ya Brazil na Ubelgiji lakini hakucheza.
No comments:
Post a Comment