SEKTA YA UJENZI YACHANGIA ASILIMIA 14 PATO LA TAIFA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, May 29, 2024

SEKTA YA UJENZI YACHANGIA ASILIMIA 14 PATO LA TAIFA


Sekta ya Ujenzi imekuwa ikikua kwa wastani wa asilimia 12 kwa mwaka kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita.

Haya yamebainishwa na Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa wakati wa kuwasilisha makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2024/25, Bungeni Jijini Dodoma

Amesema wastani wa mchango wa Sekta katika Pato la Taifa katika kipindi cha miaka 10 kuanzia mwaka 2012 hadi 2022 ni asilimia 14.

“Serikali imekuwa ikitenga fedha nyingi kila mwaka kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ambayo inatekelezwa na makandarasi kutoka ndani na nje ya nchi.“

No comments:

Post a Comment