SUNAK AAHIDI KUWAPELEKA JESHI VIJANA KWA LAZIMA. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, May 27, 2024

SUNAK AAHIDI KUWAPELEKA JESHI VIJANA KWA LAZIMA.

Waziri Mkuu wa Uingereza, Rishi Sunak.

Waziri Mkuu Rishi Sunak ameahidi kurejesha fomu ya utumishi katika jeshi la taifa kwa mara ya kwanza katika zaidi ya miaka 60.


Vijana wote wenye umri wa miaka 18 nchini Uingereza watalazimika kufanya mwaka mmoja wa utumishi wa lazima katika jeshi au kuhudumu katika jeshi la taifa kiraia, kama chama tawala cha Conservative kinashinda uchaguzi wa kitaifa wa Julai 4, chama hicho kilisema Jumapili.


Waziri Mkuu Rishi Sunak ameahidi kurejesha fomu ya utumishi katika jeshi la taifa kwa mara ya kwanza katika kipindi cha zaidi ya miaka 60, akilenga kuimarisha kampeni zake za uchaguzi baada ya kuanza vibaya. 

Uingereza ilianzisha usajili wa jeshi kwa wanaume na baadhi ya wanawake wakati wa Vita Kuu vya Pili vya Dunia, na kuweka miezi 18 ya huduma ya lazima ya jeshi kwa wanaume, kati ya 1947 na 1960.


Tangu wakati huo, Uingereza imekuwa na jeshi la kujitolea ambalo ukubwa wake umepungua kwa kasi. 



Chini ya mpango huo, kundi dogo la vijana wenye umri wa miaka 18 wapatao 30,000 kati ya 700,000 watatumika kwa miezi 12 katika jeshi, kufanya kazi katika maeneo kama vile mikakati au ulinzi wa mitandao. 



Wengine watatumika wikiendi moja kwa mwezi wakifanya kazi za misaada, makundi katika jamii, au taasisi kama hospitali, polisi na huduma ya zima moto.

No comments:

Post a Comment