TANZANIA MWENYEJI WA KILELE CHA SHINDANO LA KWANZA LA VIJANA AFRIKA KWENYE MASUALA YA AKILI MNEMBA NA ROBOTI. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, May 17, 2024

TANZANIA MWENYEJI WA KILELE CHA SHINDANO LA KWANZA LA VIJANA AFRIKA KWENYE MASUALA YA AKILI MNEMBA NA ROBOTI.


Na Carlos Claudio, Dodoma.

Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari pamoja na tume ya TEHAMAimetoa taarifa kuwa Tanzania itakuwa mwenyeji wa kwanza wa kilele cha shindano la vijana barani Afrika kwenye masuala ya teknolojia zinazoibukia (Emerging Technologies).

 

Hayo yameelezwa leo Mei 17, 2024 jijini Dodoma na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Bw. Mohamed Khamis Abdulla ambapo amesema utekelezaji wa majukumu ya ukuaji wa TEHAMA yamekuwa yakifanyika kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa sekta za umma, binafsi, mashirika ya kitaifa na kimataifa.

 

Amesema Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari imepewa jukumu la kusimamia ukuaji na uendelezaji wa sekta ya TEHAMA ambao usimamizi huo unaendana na uanzishwaji wa sera, sheria, miongozo pamoja na mikakati mbali mbali inayohusu masuala na mabadiliko ya ukuaji wa TEHAMA itakayowezesha matumizi salama na yenye manufaa ya Teknolojia zinazoibukia.

 

Ili kujenga rasilimali watu endelevu, Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na taasisi zilizo chini yake imekuwa ikiandaa programmbalimbali ikiwemo makongamano ya wataalamu wa TEHAMA ili kujadili masuala ya kuendeleza ujuzi wao katika eneo la teknolojia zinazoibukia akili mnemba, robotiki na kadhalika,”

 

Na kuongeza kuwa, “Umoja wa Afrika (AU) umeandaa makakti wa kukuza matumizi sahihi ya akili mnemba, ambapo nchi mbalimbali zimekuwa zikishiriki katika kuandaa mkakati huo ambapo umoja wa Afrika (AU-New Partnership for Africas Development) pamoja na taasisi ya ELEVATE AI ni wadau wakuu walioshiriki kuandaa mkakati huo.

 

Aidha amesema kuwa katika kutekeleza mkakati huo, nchi wanachama wanapaswa kuhamasisha ubunifu wa vijana kwenye masuala ya teknolojia zinazoibukia ikiwemo masuala ya akili mnemba.

 

Sambamba na hayo bw. Abdulla amejulisha umma kuwa mwaka huu 2024, Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kwa kushirikiana na Umoja wa Afrika (AU) na Taasisi ya Ele Vate AI, imeanza maandalizi ya kongamano la vijana wa Afrika kuonesha bunifu zao na kushindana kwenye maeneo ya masuala ya akili mnemba. 

 

Amesema kumeandaliwa shindano linalohusisha vijana ambalo lilifunguliwa tarehe 29 Februari, 2024 kupitia tovuti ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Tume ya TEHAMA pamoja na tovuti ya www.ele-vate.co.za/competition ambapo shindano hillitafungwa tarehe 08 Julai, 2024 na washindi watatangazwa tarehe 31 Agosti, 2024. 

 

Aidha Katibu mkuu huyo amesema katika shindano hilo maeneo yatakayishindanishwa ni AI and Innovation in MiningFuturist FinTech SolutionRobotics DesignAI and Robotics HealthcareEducationEnhancemnenntEthical AI, AI and Robotics Agricultural SolutionsCommunity Impact and Good GovernanceInnovations in Constructions and Artecture Industry pamoja na Open Category.

 

Ninapenda kuwajulisha kuwa washindi wa shindano hili watakabidhiwa zawadi wakati wa kilele cha kongamano la 8 la wataalamu wa Tehama Tanzania (TAIC) la mwaka 2024 litakalofanyika kuanzia tarehe 13 hadi 17 Oktoba,2024 nchini Tanzania.

 

Amesema kongamano hilo litakuwa la kipekee tofauti na makongamano mengine yaliyopita na wananchi wataweza kuona robot wengi ambao watakuwa wanaweza kujibu wasawli mbali mbali .

 

Pia amewatangazia vijana wa kitanzania, kampuni za ubunifu na jumuiya zinazohusika na masuala ya akili mnembkushiriki kwa wingi kwenye shindano hilo ili kudhibitisha utambulisho wa uwezo wa watanzania katika ramani ya wabunifu wa akili mnemba na robotics barani Afrika na duniani kote.







No comments:

Post a Comment