SERIKALI imesema kuwa barabara ya mbalizi-shigamba inayounganisha mkoa wa songwe pia mkoa wa mbeya kwa maana ya wilaya ya mbeya na wilaya ya ileje ipo kwenye hatua za manunuzi na itajengwa kwa awamu.
Hayo yameelezwa Bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Ujenzi Mhandisi Godfrey Kasekenya alipokuwa akijibu swali lililoulizwa na Mbunge wa Mbeya Vijini Oran Njenza alipouliza kuwa
Je, nilini Serikali itaanza ujenzi wa kiwango cha lami barabara ya mbalizi-shigamba.
"Mheshimiwa Naibu spika barabara hii ya mbalizi-Shigamba ambayo inaunganisha mkoa wa songwe pia na mkoa wa mbeya kwamaana ya wilaya ya mbeya na wilaya ya Ileje ipo kwenye hatua za manunuzi na tutajenga kwa awamu,
Lengo ni kuunganisha mbalizi-shigamba na itumba ileje,Tayari tupo kwenye hatua za manunuzi kwa maana ya hatua za kwanza kwa kiwango cha lami,"amesema Naibu huyo.
No comments:
Post a Comment