UONGOZI BMH WATUA NCHI ZA EAC - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, May 31, 2024

UONGOZI BMH WATUA NCHI ZA EAC


Dkt. Alphonce Chandika, Mkurugenzi Mtendaji Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) akiambatana na baadhi ya wataalamu kutoka BMH wametembelea baadhi ya nchi wanachama wa Afrika Mashariki (EAC).

"Tumekuja kwa mambo mawili, moja ni kuhudhuria vikao tulivyoalikwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki ambavyo vinalenga kujadiliana uanzishwaji wa Kituo cha Umahiri cha upandikizaji Uloto, pili tumekuja kuitangaza huduma ya upandikizaji Uloto inayotolewa na Hospitali ya Benjamin Mkapa pekee katika ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati." amesema Mkurugenzi Mtendaji wa BMH.

Mkurugenzi Mtendaji pamoja na wataalamu wa BMH wametembelea nchi za Rwanda, Burundi, Kenya na Uganda. Hospitali ya Benjamin Mkapa imeendelea kuanzisha huduma mpya zitakazo nufaisha watanzania na Afrika kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment