BARABARA ZINAZOUNGANISHA STESHENI ZA SGR KUJENGWA KIWANGO CHA LAMI. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, June 10, 2024

BARABARA ZINAZOUNGANISHA STESHENI ZA SGR KUJENGWA KIWANGO CHA LAMI.


Na Saida Issa, Dodoma 

SERIKALI imesema iko katika hatua mbalimbali za kujenga kwa kiwango cha lami barabara zote zinazounganisha stesheni za Reli ya SGR.


Hayo yameelezwa Bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Ujenzi Godfrey Kasekenya alipokuwa akijibu swali lililoulizwa na Mbunge wa kibaha vijijini Michael Mwakano alipouliza Je, Serikali haioni umuhimu wa ujenzi wa vipande vya barabara za lami kuunganisha Barabara Kuu na Reli ya SGR kwa lengo la kurahisisha wasafiri kufika Stesheni.


"Kwa sasa tumeanza na stesheni zote za kutoka Dar es salaam hadi Dodoma ambapo ujenzi wa Reli ya SGR uko katika hatua za mwisho,


Mheshimiwa Spika, kwa upande wa Mkoa wa Pwani, taratibu za manunuzi ya ujenzi wa barabara ya Mlandizi – Ruvu SGR (km 22) ziko hatua za mwisho,"amesema Naibu huyo.

No comments:

Post a Comment