MAAFISA ugavi serikalini wametakiwa kuwa wazalendo kwa kutoshindanisha wazabuni wasiokuwa na sifa ambao wamekuwa na tabia ya kutofikisha huduma na bidhaa zenye ubora kwa mujibu wa mkataba ikiwa ni pamoja na bei ya bidhaa isiyokuwa ya soko.
Hayo yamesemwa hivi karibuni na Mkurugenzi Mtendaji Halmshauri ya jiji la Mbeya Bw. John Nchimbi wakati akifungua Mafunzo ya Mfumo wa Ununuzi wa Umma kielektroniki NeST kwa taasisi mbalimbali za umma za mikoa ya mbeya, Rukwa na Mtwara yaliyoendeshwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA).
Bw. Nchimbi amesema kuwa Serikali ya awamu ya sita ina nia njema sana na wananchi wake na kwamba imetengeneza mazingira rafiki kwa raia wake ili kunufaika na fursa zilizopo kupitia Ununuzi wa Umma.
Nawasihi kuwa wazalendo ili kuipunguzia mzigo serikali na kuwezesha miradi kukamilika kwa wakati kwani miradi hii itakapokamilika kwa wakati na ubora wake itatufaa sisi Wananchi" amesema Bw. Nchimbi
Meneja wa PPRA kanda ya nyanda za juu kusini Paschal Manono amesema kuwa moja ya changamoto ya kufanya michakato ya Ununuzi nje ya Mfumo ukiachilia suala la faini changamoto nyengine ni utangazaji wa tenda kwa gaharama kubwa isiyoendana na ushindani na kuisababishia suala linalopelekea Serikali kupata hasara.
No comments:
Post a Comment