Mahakama Kuu jijini Nairobi leo inatarajiwa kusikiliza kesi iliyowasilishwa na Chama cha Wanasheria nchini (LSK) kupinga hatua ya Bunge kuidhinisha Jeshi la Ulinzi la Kenya KDF kusaidia polisi kudumisha kufuatia maandamano mabaya ya kupinga nyongeza ya kodi mnamo tarehe 25 Juni.
LSK, kupitia kwa rais wake Faith Odhiambo, siku ya Jumanne iliomba mahakama isitishe uamuzi huo baada ya Waziri wa Ulinzi Aden Duale, kwenye notisi ya gazeti rasmi la serikali mnamo tarehe 25 Juni, kusema kuwa jeshi lilikuwa limetumwa kusaidia polisi kuzima maandamano hayo yenye ghasia.
Mawakili hao walimshtumu Duale na Bunge la Kitaifa kwa kukiuka sheria kwa kupeleka jeshi kinyume cha sheria ili kudumisha sheria na utulivu, jukumu ambalo limepewa polisi.
Wabunge jana waliidhinisha kutumwa kwa jeshi ili kudhibiti machafuko yaliyochochewa na mapendekezo ya nyongeza ya ushuru.
Vyombo vya habari vya ndani vinaripoti kuwa wabunge "walitofautiana vikali " katika mabishano wakati wa hoja ya kuidhinisha kutumwa kwa wanajeshi kulinda amani.
No comments:
Post a Comment