PROF. MKENDA AIPONGEZA OR-TAMISEMI KWA KUWEKEZA KWENYE MICHEZO MASHULENI. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, June 15, 2024

PROF. MKENDA AIPONGEZA OR-TAMISEMI KWA KUWEKEZA KWENYE MICHEZO MASHULENI.


OR-TAMISEMI

Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda, ameipongeza Ofisi ya Rais -TAMISEMI kwa uratibu mzuri wa mashindano ya UMITASHUMTA & UMISSETA 2024.

Prof. Mkenda ameeleza hayo leo tarehe 15 Juni 2024, wakati akizungumza kwenye sherehe za kuhitimisha mashindano ya UMITASHUMTA 2024 kwenye viwanja vya shule ya Sekondari Tabora Wavulana. 

"TAMISEMI wamefanya uwekezaji mkubwa ikiwepo kutenga shule maalum kwa ajili ya kukuza michezo ya vijana nchini, hali ambayo inaleta matumaini ya kuwa na wanamichezo bora katika siku zijazo" amesema Prof.Adolf Mkenda. 


Amesma kuwa wizara yake itaendelea kushirikiana na wizara zingine zinazohusika na michezo pamoja na elimu, ili kuweka mikakati endelevu itakayosaidia kuibua na kukuza vipaji vya watoto kupitia michezo shuleni kwa ajili ya kuandaa timu za Taifa.

Awali akizungumza kwenye sherehe hizo, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt.Rashid Chuachua, aliishukuru Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kuwezesha uandaaji wa mashindano ya UMITASHUMTA & UMISSETA Mkoani Tabora kwa miaka mitatu mfululizo. 

Dkt. Chuachua ameeleza kuwa Mkoa wa Tabora umenufaika na mashindo ya UMITASHUMTA & UMISSETA, na yameuendeleza mkoa kwa kiwango kikubwa kielimu, kimechezo pamoja na Uchumi.


Mashindano ya UMITASHUMTA & UMISSETA 2024, yanaandaliwa na kuratibiwa na Ofisi ya Rais TAMISEMI ikishirikiana na Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo pamoja na Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia.

No comments:

Post a Comment