Tumia rafiki Briquettes, okoa mazingira - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, June 21, 2024

Tumia rafiki Briquettes, okoa mazingira


Watanzania wametakiwa kutumia mkaa mbadala wa rafiki briquettes ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi yanayosababishwa na uharibufu wa mazingira.

Wito huo umetolewa afisa kutoka shirika la madini la taifa (STAMICO) bwana Ignas Mchila ambapo amebainisha kuwa rafiki briquettes ni mkaa mbadala uliochakatwa kutoka kwenye mabaki ya makaa ya mawe na kuondolewa moshi hivyo kuwa rafiki wa mazingira.

Amesema mtumiaji anauwezo wa kutumia mkaa huo kwa taklibani masaa matatu baada ya kuwasha na hivyo kuwa rahisi kwa matumizi ya majumbani na taasisi zenye mahitaji ya nishati hiyo kama mashuleni, vyuoni nakadhalika.

Kuhusu gharama Mchila amesema mkaa huo unapatikana kwa shilingi 1,000 kwa kilogramu moja na mtumiaji anaweza kutumia kidogo kidogo kulingana na ukubwa jiko lake.


STAMICO kupitia kauli mbiu “USIKATE MITI HOVYO, OKOA MAZINGIRA” imedhamiria kurahisisha upatikanaji wa rafiki briquettes nchi nzima katika kukabiliana na matumizi ya mkaa unaotokana na miti ili kutunza mazingira.

Hayo yamejili katika maonyesho ya Idodomia International Expo yanayoendelea katika viwanja vya shule ya sekondari Dodoma mkabala na bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Idodomia Expo imeandaliwa na Triprecy Initiative foundation, ofisi ya mkuu wa mkoa wa Dodoma, Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) taasisi za mbalimbali za serikali pamoja na wadau wengine.


No comments:

Post a Comment